Afya

Fahamu kuhusu ubuyu na faida zake

Kwa muda wa miaka kadhaa sasa Ubuyu umekuwa ukitajwa mdomoni mwa watu kuwa mni moja ya mmea wenye faida nyingi katika mwaili wa binadamu, pia hata unga wake unatajwa kuwa ni moja ya chanzo kikubwa kinachosaidia mwili wa binadamu usipatwe na maradhi.

Unga wa ubuyu unaelezwa kuwa na vitamini na madini mengi kuliko matunda mengine yoyote unayoyajuwa.

1. Inaelezwa kuwa unga wa ubuyu una vitamini C nyingi mara 6 zaidi ya ile inayopatikana katika machungwa.

2. Ubuyu una kiwango kingi cha madini ya Kashiamu (Calcium) mara 2 zaidi ya maziwa ya ng’ombe, pia madini mengine yapatikanayo katika ubuyu ni pamoja na madini ya Chuma, Magnesiamu na Potasiamu ambayo ni mara 6 zaidi ya ile potasiamu ipatikanayo katika ndizi.

3. Husaidia kujenga neva za fahamu mwilini

4. Ina virutubisho vya kulinda mwili

5. Ubuyu una vitamini B3 na B2 ambayo ni mhimu katika kuondoa sumu mwilini na umeng’enyaji wa madini ya chuma, kimsingi vyakula vyenye afya zaidi kwa ajili ya mwili ya binadamu huwa pia huwa na vitamin B2.

6. Unaongeza kinga ya mwili sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamini C

7. Huongeza nuru ya macho

8. Husaidia kuzuia kuharisha na kutapika

9. Ina magnesiam ambayo husaidia kujenga mifupa na meno

10. Husaidia wenye presha ya kushuka na wenye matatizo ya figo

Hakikisha kuwa kila siku unapata glasi moja ya juisi ya ubuyu hasa usiku na baada ya wiki kadhaa utaona matokeo yake mwilini. Na ili upate faida za juisi ya ubuyu, zinazoelezwa hapa, lazima upate ule ubuyu halisi (mweupe) usiochanganywa na kitu kingine cha kuongeza ladha au rangi.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents