Technology

Fahamu: Kupatikana chanjo ya shambulio la mitandaoni

Watafiti wa usalama mtandaoni wamegundua chanjo ya shambulio la uhalifu wa mitandaoni lililoathiri mashirika tofauti duniani siku ya Jumanne lakini haijajulikana shambulio hilo lilitoka wapi na lengo lake ni nini.

Baadhi ya waathiriwa wa shambulio hilo la siku ya Jumanne ni benki kuu ya Ukraine, kampuni kubwa ya mafuta kutoka Urusi Rosnet, kampuni ya matangazo ya Uingereza WPP, hospitali moja ya Marekani katika mji wa Pittsburgh na kampuni ya mawakili wa Marekani DLA Piper.

Sasa basi, kwa kutengeza faili kwa jina Perfc na kuiweka katika “C:\Windows” folder, shambulio linaweza kusitishwa mara moja. Hata hivyo huku mbinu hiyo ikiwa ina uwezo wa kudhibiti kirusi hicho, ina uwezo wa kuzilinda kompyuta za kibinafsi ambazo faili zina Perfc lakini watafiti wameshindwa kupata suluhu ya kudumu.

Kwa watumizi wengi, kuweka Windows mpya ni suluhu ya kuzuia shambulio hilo iwapo ingetaka kuathiri komyuta yako.

Kusambaa kwa kirusi hicho kipya kunaweza kuwa kwa mwendo wa pole ikilinganishwa na kile cha mwezi ulioipita cha WannaCry wataalam wametabiri huku wachangunuzi wa alama za siri wakisema kuwa kirusi hicho hakikuwa na lengo la kusambaa zaidi ya lengo lake.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents