Fahamu: Lady Jaydee na Alicios walishawahi kutumbuiza jukwaa moja

Msanii Alicios kutoka Congo DRC ambaye anafanya kazi zake za muziki nchini Kenya, amekuwa akimzimia malkia wa Bongo Flava, Lady Jaydee kwa kipindi kirefu mpaka sasa wamebahatika kusimamiwa katika menejimenti moja ya Taurus Musik.

Je umeshawahi kuwaona wasanii hao wakitumbuiza katika jukwaa moja? Basi nakufahamisha kuwa wasanii hao walishawahi kufanya hivyo tena mara moja pekee.

Bahati hiyo ilitokea nchini Kenya ambapo walifanya show kwenye tamasha la United Sound Of Africa (USA) ambalo liliwakutanisha wasanii takribani 15 akiwemo Runtown kutoka Nigeria na Aika na Nahreel.

Wasanii hao wanatarajiwa kutumbuiza tena pamoja kwenye sherehe za sikukuu ya Valentine’s Day, February 10 ya mwaka huu katika ukumbi wa Serena Hotel.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW