Fahamu

FAHAMU: Leo Bob Marley angetimiza miaka 74 kama angekuwa hai, hii ndio historia yake

Robert Nesta “Bob” Marley alizaliwa siku kama ya leo February 6 mwaka 1945 katika kijiji cha Nine Mile kwenye Parishi ya mtakatifu Ann huko Jamaica. Wakati akiwa mdogo, marafiki zake walimpa jina la utani la ‘Tuff Gong’.

Image result for bob marley
Bob Marley

Mama mzazi wa Bob Marley alikuwa ni Mjamaica mweusi aliyeitwa Cedella Booker.

Historia ya maisha yake haitofautiani sana na wanamuziki wenzake wa reggae Peter Tosh aliyelelewa na shangazi yake na Bunny Wailer aliyelelewa na baba yake. Historia ya huzuni iliyo muacha Bob Marley chini ya mzazi mmoja (mama yake) pale alipofiwa na baba yake akiwa na umri wa miaka 10.

Norval Sinclair (baba yake Bob Marley) alikuwa nahodha wa meli na muangalizi wa mashamba alifariki mwaka 1955 akiwa safarini, wakati huo alikuwa na umri wa miaka 60.

Kifo hicho kilimfanya mama yake Bob Markey ahamishie makazi kwenye mji wa Kingston, huko Bob alikutana na Bunny Wailer wakawa marafiki na kujifunza muziki pamoja. Muda huo akiwa na umri wa miaka 14.

Bob Marley alianza muziki miaka ya 1960 akiwa na kundi lake la The Wailers, ambalo alilianzisha akiwa na marafiki zake Peter Tosh na Bunny Wailer.

Bob alifanikiwa kupata watoto wanne na aliyekuwa mke wake, Bi. Rita Anderson aliyemuoa mwaka 1966 na moja ya watoto hao ni Ziggy Marley, ambaye pia ni mwimbaji wa reggae maarufu nchini Marekani.

Kwa mujibu wa maelezo kutoka kwenye tovuti rasmi ya Bob Marley ameacha watoto 11 kwa wanawake tofauti tofauti .

Licha ya kundi hilo la The Waillers kuvunjika, Mwaka wa 1974 Bob Marley aliendelea kuita bendi yake jina la Bob Marley and the Wailers na kujiunga upya na wanachama wapya huku wakiendelea kupiga muziki kama kawaida.

Mwaka wa 1975,  Bob Marley akatoa wimbo wake wa kwanza ambao ulimpa umaarufu duniani kote, ulijulikana kama “No Woman No Cry”.

Baadhi ya nyimbo zake kali ni pamoja na “I Shot the Sheriff”, “Could You Be Loved”, “Stir It Up”, “Jamming”, “Redemption Song”, “One Love” na, “Three Little Birds”.

Bob Marley alifariki mwaka 1981 katika hospitali ya Cedars of Lebanon mjini Miami, nchini Marekani kwa kansa ya ngozi.

Je, ni ngoma gani ya Bob Marley ambayo hadi leo ukiisikiliza unaona kama wimbo mpya kwenye masikio yako?

REST IN PEACE BOB MARLEY

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents