Fahamu

Fahamu mambo sita kutoka kisiwa cha Guam, Marekani

Kisiwa cha Guam ni kisiwa kukubwa kilichopo katika bahari ya Pacific nchini Marekani.

  1. Licha kumilikiwa na Marekani, kisiwa hicho kipo umbali wa maili 8,000 na inachukua takriban saa 19 kukifikia kisiwa hicho kwa usafiri wa ndege kutoka mji wa New York. Wamarekani wanaweza kuingia katika kisiwa hicho bila kutumia pasipoti.

2. Raia wa eneo hilo ni wa Marekani lakini hawawezi kupiga kura ya kumchagua Rais wa Marekani, piia wana mwakilishi mmoja wa serikali ingawa hana uwezo wowote kuhusu utungaji wa sera.

3. Robo ya kisiwa hicho kinamilikiwa na jeshi la Marekani na kinatumiwa kama kambi ya wanamaji na wanaanga,vile vile silimia 10 ya watu wa Guam ni wanajeshi.

4. Raia wa Guam wanajulikana kama Chamorro, utamaduni wao unafanana na ule wa Uhispania zaidi ya Umarekani kwa sababu Uhispania ilidhibiti kisiwa hicho kwa takriban miaka 300.

5. Watu katika eneo hilo hawatozwi kodi pia maduka huuza bidhaa za mitindo na hufunguliwa kwa muda wa saa 24 kwa siku.

6. Ricardo Blas Jr. ndio mtu maarufu zaidi katika kisiwa cha Guam, mtu huyu hucheza mchezo wa judo katika michezo ya Olimpiki ya 2008 na 2012 na alibeba bendera ya Guam katika mashindano.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents