Burudani
Fahamu maproducer 12 waliohusika kupika albamu ya ‘KISIMANI’ ya Wakazi
Rapper Wakazi ameachia orodha ya maproducer waliotengeneza albamu yake ya ‘Kisimani’ yenye ngoma 18.
Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram wa Wakazi ameweka orodha ya maproducer hao takribani 12 na kuelezea kila mmoja ngoma aliyofanya.
Maproducer hao ni:-Kzthesoulplugger aliyetayarisha ngoma mbili ambazo ni ‘Matatizo’ pamoja na ‘Pole Pole Bro’, Marco Chali aliyetayarisha ngoma ya ‘Nimezama’, Bigg Stickerz huyu katayarsiha ngoma ya ‘Mtu Mzima’, Producer mwingine ni Palla Midundo ambaye ametayarisha ‘Hapa Wakazi Tu’ ,pia producer aitwaye Calidro yeye ametengeneza wimbo wa ‘Nimetekwa’.
Pia kuna maproducer kama vile John Mahundi, Will HD Masanja, Banostylez, Cjamoker, Q TheDon, Abbah The Process na Mwijahuku.