Aisee DSTV!

Fahamu mastaa wanaoingiza mkwanja mrefu zaidi kwenye mtandao wa Instagram

Fahamu mastaa wanaoingiza mkwanja mrefu zaidi kwenye mtandao wa Instagram

Muanzilishi wa mtandao wa HopperHQ.com, ambao unadili na masuala ya uchambuzi wa data mbalimbali za Instagram, Mike Bandar amesema kuwa mtandao huo umekuwa nizaidi ya mawasiliano kwa hivi sasa hadi kupelekea wanamichezo na watu wengi mashuhuri kujipatia fedha nyingi kupitia matangazo ya biashara wanayo weka.

Mwanadada Kylie Jenner

Bandar amesema kuwa kutokana na idadi kubwa ya mashabiki wanao wafuatilia watu wanao wapenda kupitia mtandao huo wa Instagram inawafanya watu hao mashuhuri kujipatia mkwanja mrefu.

Kwa mujibu wa uchambuzi wa mtandao huo wa HopperHQ.com, umetoa ripoti ya wanaongoza kuwa na namba kuwa ya mashabiki kwenye Instagram na mkwanja ambao wanaingiza kwa tangazo moja pekee.

Anayeongoza kwenye orodha hiyo ni mwanadada Kylie Jenner mwenye umri wa miaka 20, ambaye anakusanya dola za Kimarekani milioni moja kwa kila tangazo moja analoposti kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram akiw na ‘followers’ milioni 111.

Uchambuzi huo umemtaja mchezaji bora dunia, Cristiano Ronaldo akishika nafasi ya tatu akiwa anavuta kiasi cha dola za Kimarekani milioni  750,000 akiwa na ‘followers’ 136 kwenye mtandao wake wa Istagram huku akishika nafasi ya kwanza kwa upande wa wanasoka.

Selena Gomez mwenye ‘followers’ wengi zaidi duniani milioni 139 ameshika nafasi ya pili kwa kuvuta mkwanja mrefu zaidi kwenye mtandao huo wa Instagram.

Na hawa ndiyo wanaoongoza kwa upande wa mchezo wa soka duniani, mshambuliaji wa klabu ya Juventus Cristiano Ronaldo ambaye anashika nafasi ya pili duniani kwa kuwa na ‘followers’ wengi kwenye mtandao wa Instagram anakusanya dola za Kimarekani milioni 750,000.

Nafasi ya pili inashikiliwa na mshambuliaji wa Brazil na klabu ya PSG, Neymar ambaye anaondoka na kiasi cha dola za Kimarekani 600,000 kwa tangazo moja tu analoweka kwenye mtandao huo wa Instagram akiwa na ‘followers’ 100.

Image result for neymar

Mshambuliaji wa Argentina, Lionel Messi mwenye ‘followers’ 97.3 kwenye Instagram anaingiza dola milioni 500,000 kwa tangazo moja tu analoposti.

Nafasi ya nne kwenye mchezo huo wa soka inachukuliwa na Beckham raia wa Uingereza mwenye ‘followers’ 49.7 kwa kukusanya dola milioni 300,000 wakati  ya tano ikienda kwa Bale mwenye ‘followers’ 35 akiingiza dola milioni 185,000 kwa tangazo moja analorusha kwenye Istagram yake.

Related Articles

3 Comments

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW