Soka saa 24!

Fahamu mataji, tuzo na rekodi alizoziweka Ronaldo akiwa na Real Madrid kabla ya kujiunga na Juventus

Habari mbaya zaidi kwa mashabiki wa Real Madrid kwa siku ya leo ni kwamba mshambuliaji wao tegemezi, Cristiano Ronaldo ametangaza rasmi kuiaga klabu hiyo na kujiunga na klabu ya Juventus kwa dau linalotajwa kuwa ni Euro milioni 105.

Image result for Ronaldo best moments
Cristiano Ronaldo

Tuangalie rekodi mbali mbali alizoziweka akiwa na Real Madrid tangu ajiunge na klabu hiyo mwaka 2009 akitokea Manchester United.

->Ronaldo ameondoka Real Madrid akiwa ameifungia magoli 450 kwenye michuano yote huku akiwa amecheza mechi 438 pekee na ndiye mfungaji wa magoli mengi ndani ya klabu hiyo kwa muda wote.

->Akiwa na Real Madrid Ronaldo ameshinda mataji 16 manne yakiwa ni ya Klabu Bingwa, matatu ya Kombe la Dunia la Vilabu, mawili ya La Liga, mawili ya kombe la Mfalme (Cpo Del Rey), mawili ya ngao ya hisani na mawili ni ya UEFA Super Cup.

->Ronaldo akiwa na Real Madrid pia amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia mara nne.

->Ronaldo pia maechukua tuzo ya mchezaji bora barani Ulaya mara tatu akiwa na Real Madrid.

Hizo ni baadhi ya rekodi na mataji aliyochukua Cristiano Ronaldo akiwa na Real Madrid na ikumbukwe mshambuliaji huyo akiwa na miaka 24 aliuzwa kwa dau la Euro milioni 89 mwaka 2009 na kwa kipindi hicho ndio lilikuwa dau kubwa zaidi la kihistoria.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW