Michezo

Fahamu mechi 15 za Aston Villa zinazomtegemea Mbwana Samatta – Video

Fahamu mechi 15 za Aston Villa zinazomtegemea Mbwana Samatta - Video

Klabu ya Aston Villa imethibitisha kumsajili mshambuliaji Mbwana Samatta kwa mkataba wa miaka minne na nusu kuitumikia klabu hiyo hadi mwezi Juni, 2024.

Usajili huo umekamilishwa kwa ada ya Pauni milioni 8.5 na moja kwa moja ataingia katika kikosi kinachojiandaa na mchezo wa ligi leo Jumanne, Januari 21 dhidi ya Watford japokuwa kuna uwezekano mdogo wa kuanza kwenye kikosi cha kwanza.

Kwangu mimi ina maana kubwa sana, nchini Tanzania watu wanapenda soka na wanapenda kuangalia Premier League. Itakuwa ni kipindi ambacho Watanzania wanakwenda kumuangalia mchezaji wao akiichezea Aston Villa“, amesema Samatta katika mahojiano yake ya kwanza na mtandao wa klabu hiyo.

Kuelekea kwenye kampeni ya ligi na michuano mingine, Samatta atakuwa na kibarua kuanzia wikiendi hii ambapo katika mechi 10 za kwanza, Aston Villa itacheza na Watford (H), Leicester City (H), Bournemouth (A), Tottenham Hotspurs (H), Southampton (A), Sheffield United (H), Chelsea (H), Newcastle United (A), Wolverhampton (A), Liverpool (A), Manchester United (H), Crystal Palace (H), Everton (A), Arsenal (H), West Ham (H).

Aston Villa inakamata nafasi ya 18 katika msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza, ikiwa imeshinda mechi sita, imefungwa mechi 13 na sare nne ikiwa na alama 22 na ikiwa katika nafasi hiyo inatarajiwa kupigania ili isishuke daraja kwani ipo kwenye mstari mwekundu wa kushuka daraja na Samatta ndio mshambuliaji pekee atakayetarajiwa kunyanyua matumaini ya Aston Villa ili waendelee kubaki katika ligi hiyo.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents