Michezo

Fahamu michezo mitano ambayo huenda hujawahi kuisikia 

Kunamichezo mingi katika ulimwengu huu, ipo unayo ijua na mengine huwanda uifahamu kabisa na hii ni baadhi tu inayo kuja kwa kasi na kujiongezea mashabiki wengi duniani kote.

Chess Boxing huu ni mchezo wa masumbwi unao changanyika na mwingine ndani yake unaitwa Chesse, ukiungananisha ndipo unapopata Chesse Boxing.

Mabondia hupigana raundi 11 ulingoni huku katika mizunguko yote hiyo hupata nafasi ya dakika tatu kupigana na tatu ya kucheza Chesse hambapo hutumia kete za rangi mbili tofauti.

Mechi kubwa kupata kutokea ilifanyika Berlin mwaka 2003 na toka hapo dunia ilishindwa kuamini kwa kile kilichotokea na watu kuanza kuufatilia kwa karibu mchezo huu.

Kwa sasa Chess Boxing umekuwa mchezo rasmi India, Ujerumani, Uingereza, Urusi na baadhi ya nchi huku ukizidi kujiongezea mashabiki.

Wife Carrying ni mchezo ambao umeanzishwa huko Finland sasa kujizoelea umaarufu sehemu mbalimbali duniani kwa sasa.

Mchezo huu wa Wife Carrying huchezwa pale mume anapo mbeba mkewe na kukimbia naye umbali wa mita 253  huku mwanaume akikutana na changamoto mbalimbali katika mbio hizo ikiwemo kupita kwenye madimbwi ya maji, kuruka viunzi, milima na mabonde huku mkewe akiwa mgongoni na mwisho mshindi kupatikana.

Extreme Ironing ni mchezo uliyobuniwa Leicester  mwaka 1997  ambapo wenyewe hauna sehemu maalumu ya kuchezwa bali popote pale.

Huwenda ukachezwa sehemu kavu, kwenye milima, ama hata ndani ya bahari ambapo kila mshiriki hutumia pasi kunyoosha ngu bila kujali mazingira uliyopo.

Toe Wrestling wenye ni mchezo ambao hautofautiani sana na ule wa kupimana ubavu ama nguvu kwa kushikana mikono.

Tofauti ya mchezo huu washiriki hutumia miguu kupimana nguvu kwa kuvinasisha vidole gumba kisha mwamuzi kuhisabu na shindano kuanza huku sharti ni lazima kuvua viatu.

Wakati mchezo wa mwisho tunao kuletea ambao huwenda hujawai kuhufahamu ni Sauna World Championships wenye ukipata umaarufu mkubwa Finland miaka 1999 hadi 2010.

Mchezo huu huchezwa na jinsia zote wanaume na wanawake ikiwa na idadi ya watu sita ambao hukaa kwenye chumba kidogo maarufu kama ‘Sauna’ na kuwekewa joto kali mno huku likiongezwa kadri washiriki wanavyo vumilia mpaka mshindi kupatikana.

Mwaka 2010 ilipata kushudiwa mmoja kati ya washiriki aliyefika hatua ya fainali, Vladimir Ladyzhensky akipoteza maisha kutokana na joto kali lililokuwemo kwenye chumba hicho.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents