Fahamu

Fahamu: Mke wa Rais wa Ufaransa aliyekua mwalimu wake wa sekondari

Emmanuel Macron, mwenye umri wa miaka 39, ndiye rais mpya wa taifa la barani ulaya, Ufaransa aliyepitwa miaka 25 na mkewe
Baada ya kuwania kiti cha urais huo, maisha ya Macron, yameanza kuwa kivutio kwa watu wengi hasa wale wadakuzi wa mambo. Imefahamika kwamba, mke wake ana miaka 64, huku Macron akiwa na miaka 39. Ndoa yao inayosisimua na kushangaza watu mbalimbali kwani chanzo cha wawili hao kukutana ni mmoja alikua mwalimu, Macron, na mkwewe Brigitte, mwalimu wake.

Kitaalumu Brigitte Trogneux yaani mke wa Emmanuel Macron ni mwalimu. Mwanamama huyo anabainisha kuwa alishuhudia kijana Emmanuel Macron akimpa ahadi ya kumuoa wakati akiwa na miaka 17.
Alishangaa kuona kijana mwenye umri wa miaka 17 anataka kumuoa mwalimu wake, ambaye amemzidi miaka mingi ya kuzaliwa.

Lakini hatimaye, sasa Macron na Brigitte ni wanandoa ambao sasa ndio ‘First Family’ ya Ufaransa huku Brigitte kuwa ‘First Lady’.

Macron akiwa na miaka 15 tangu azaliwe ndipo alikutana na Brigitte kama mwalimu wake. Baadaye Macron alimpa ahadi Brigitte kuwa atamuoa mwalimu huyo.
“Akiwa na umri wa miaka 17, Emmanuel aliniambia, chochote unachofanya, nakuahidi nitakuoa wewe Brigitte,” alisema Trogneux alipozungumza na jarida la Paris Match.
Uhusiano wa kimapenzi kati ya wawili hao ulianza pale Emmanuel Macron alipopewa jaribio la kuigiza tamthilia fupi iliyoandaliwa na mwalimu wake Brigitte Trogneux. Kipindi hicho Emmanuel alikuwa na miaka 18 tu na mwanafunzi wa Shule ya Shirika la Jesuit iliyopo Amiens, kaskazini mwa Ufaransa.


Mwalimu huyo ndiye alikuwa msimamizi wa jaribio la kuigiza tamthilia hiyo kwenye ukumbi wa shule.
Aidha, inaelezwa kuwa Macron alipendelea mno fasihi ambapo alitaka kuwa mwandishi wa riwaya na vitabu.
Baadaye Macron alihama kutoka Amiens kwenda jijini Paris katika mwaka wake wa mwisho wa kuhitimu sekondari.
“Kwa kipindi hicho tulipigiana sana simu. Tuliongea mengi kwa muda mrefu, tulitumia muda mwingi kuzungumza kwa simu, yaani masaa mengi tulipoteza kwenye simu,” alisema Brigitte.
Mwalimu huyo aliongeza kwa kusema, “Kidogo kidogo, alifuzu vikwazo nilivyomwekea hata sikuamini. Tena kwa utulivu na uvumilivu. Hakuwa mtoto tena. Alikuwa na mahusiano ya kimapenzi kama mtu mzima yeyote,”
Baadaye Brigitte alihamia Paris kuungana na Emmanuel Macron. Uamuzi wa kuhamia Paris uliambatana na kuachana na mumewe. Hii ina maana Brigitte alilazimika kuvunja ndoa yake ili aolewe na mwanafunzi wake.


Macron na Brigitte walifunga ndoa mwaka 2007, ingawaje hakutumia jina la mumewe badala yake alichagua kubaki na lake.
“Siwezi kumficha kitu. Yuko hapa, yeye ni maisha yangu. Daima yuko nami kwa hilo,” alisema Emmanuel Macron alipohojiwa wiki hii na French TV.
Katika hotuba yake mwezi uliopita, wanandoa hao walibusiana hadharani wakiwa ukumbini, ndipo Macron aliwaambia wafuasi wake, “Ninamhusudu kupindukia Brigitte, kwasababu amenifanya niwe mtu mwenye hadhi na heshima ninavyoonekana leo,”
Kisha alimgeukia mkewe na kumwambia, “Usikae nyuma yangu. Tukichaguliwa, hakuna kubaki nyuma. Tukichaguliwa, atakuwa na majukumu kuitumikia Ufaransa.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents