Habari

FAHAMU: Mwaka mmoja umepita tangu Mhe. Tundu Lissu ashambuliwe kwa risasi jijini Dodoma (+video)

Mnamo tarehe 7 Septemba 2017, aliyekuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Mhe. Tundu Lissu akiwa maeneo ya Area D mjini Dodoma alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana.

Tundu Lissu baada ya tukio hilo alipelekwa katika Hospitali ya General na baadae kusafirishwa jijini Nairobi kwa kupatiwa matibabu zaidi.

Hata hivyo, Tundu Lissu baadae alitolewa tena nchini Kenya na kwenda kutibiwa nchini Ubelgiji huku sababu za  kiusalama zikitajwa kusafirishwa kwake.

Kwa mujibu wa maelezo yake, mpaka sasa Tundu Lissu ametolewa risasi zaidi ya 10 na kufanyiwa upasuaji mara 21 kwenye mwili wake na hali yake imeendelea kuimarika siku hadi siku.

Akizungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Mhe. Lissu amedai kuwa tangu aanze matibabu nchini Kenya na Ubelgiji hajapata fedha za matibabu kutoka Bungeni.

Akizungumza zaidi kwenye mahojiano yake na BBC, Tundu Lissu amesema kuwa mpaka sasa hajahojiwa na jeshi la polisi wala Afisa yoyote wa Bunge ambaye ameenda kumtembelea kumjua hali.

Kwa upande mwingine mapema mwaka jana baada ya tukio hilo la Lissu, Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro, alisema kuwa jeshi la polisi badolinafanya upelelezi na anahitaji ushirikiano wa raia wema kutoa taarifa.

Mpaka sasa Jeshi la Polisi bado linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo, huku Mhe. Tundu Lissu mwenyewe akikiri wazi kuwa bado hajawabaini kwa sura watu hao waliomshambulia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents