Afya

Fahamu namna ya kuepuka kunuka kinywa/mdomo

Kitendo cha kutoa harufu mbaya mdomoni ni kitendo kinachoweza kuathiri mahusiano si kwa mpenzi tu bali hata marafiki na jamii kwa ujumla.

Asilimia 85 – 90% ya tatizo la harufu mbaya mdomoni asili yake ni kinywa chenyewe. Pia kiwango cha harufu hutofautiana kutokana na muda (mchana, usiku na asubuhi).

Kutokuwa makini na usafi wa kinywa kama vile kupiga mswaki vizuri kwa kuacha mabaki ya chakula ambayo huoza na kusababisha harufu mbaya mdomoni ni moja ya chanzo kikubwa kinachotajwa kusababisha harufu mbaya mdomoni.

Ni vigumu kwa haraka haraka kutambua kama unatoa harufu katika kinywa chako ila unaweza kutambua kwa kumuuliza mtu unayemuamini. Pia unaweza kujua harufu mbaya kwa kulamba nyuma ya kiganja na kunusa, wengine hupumua mbele ya kioo na kunusa. Pia unaweza kutumia kijiti cha kuchokonolea meno na kukinusa. Kisayansi unaweza kutumia vifaa kama Halimeter, Gas Chromatography na BANA Test.

Waswahili wanasema Kinga bora kuliko tiba hivyo basi unaweza kufanya yafuatayo kukomesha adha hiyo:-

  • Kupiga mswaki – Unatakiwa upige mswaki mara mbili kiafya asubuhi na kabla ya kulala, ila unashauriwa pia kupiga mswaki ukimaliza kula chakula chako ili kuondoa mabaki ya chakula kwa muda huo.
  • Kunywa maji mengi – Unywaji wa maji ya kutosha kila siku utakusaidia kudhibiti na hatimaye kuondoa tatizo la kunuka mdomo. Unywaji wa maji mengi ni muhimu, hasa kwa wale watu wenye ugonjwa wa kukauka midomo (xerostomia).

Zingatia kunywa maji mengi sana  kwani unywaji wa maji husaidia kuondoa tatizo la kutoa harufu mbaya mdomoni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents