Fahamu ngoma zenye historia katika maisha ya Diamond

Wakati dunia ikisubiria kuisikiliza kwa mara ya kwanza albamu ya pili ya msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz iitwayo ‘A BOY FROM TANDALE’, msanii huyo ametaja sababu ya kuziweka baadhi ya ngoma zilizowahi kuzitoka kipindi cha nyuma.
Akiongea katika mahojiano maalumu na Bongo5, Diamond ameeleza kuwa ngoma hizo ambazo zimewahi kutoka na watu wanazijua ila zipo katika albamu zinahistoria katika maisha yake.

“Sababu kubwa ya kuweka nyimbo ambazo zimesikika kuna nyingine zina historia kubwa sana kwenye maisha yangu ambazo huwezi kuziacha tu ukizingazia albamu yangu ya mwisho ilikuwa ni Lala salama”.

“Kuna nyimbo kama Number One, Nana, Kidogo, kama Eneka ni nyimbo ambazo zina historia katika maisha yangu huwezi kuzitupa tu usiziweke, so imeniladhimu niziweke ili mtu akipata albamu yangu aweze kusikia uzuri wa zile kazi kwa sababu naamini albamu yangu itafika sehemu nyingine pengine muziki wangu haujawahi kufika.”

“Albamu mara nyingi inakuwa na nyimbo nane hadi kumi 10 na ndio imekuwa sababu maalumu ya kuweka nyimbo 20, iwe kama bonus kwa watu wengine ili wasipate tabu maana wakisikiliza albamu waende tena wakatafute nyimbo nyingine,” amesisitiza Diamond.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW