Burudani

Fahamu : Nyimbo 5 zitakazokupa matumaini wakati wote

Mara nyingi tumesikia na kutazama nyimbo nyingi za mapenzi, na huenda ikawa ndio kitu tunachokumbana nacho kila wakati ama kutuzunguka.

Hizi ni nyimbo tano tofauti zikitokea hapa bongo zinazoweza kukufariji na ukaamini kuna jambo unaweza fanya katika haya maisha.

Namba 1:Selina-Jitume

Ni msanii wa muziki bongo amewahi kufanya nyimbo ikaitwa Dollar. Baada ya nyimbo hiyo ameamua kubadili aina ya muziki na sasa anafanya Inspirational songs .

Namba 2 Goodluck Gozbert-Ipo siku

Huyu ni mtayarishaji pia wa muziki lakini kwa sasa ameamua kujikita katika uimbaji. Katika uimbaji wake Goodluck ameamua kujikita katika nyimbo za mungu, lakini ipo siku ni moja ya nyimbo zilizopendwa sana kwani haikujali wewe ni mfuasi wa dini gani.

Namba 3: Benpol-Jikubali

Jikubali ni moja ya nyimbo ambayo ilimuonesha msanii huyu katika upande mwingine, ni nyimbo inayokuhamasisha kuota ndoto zako na kuamini unaweza kuwa kama mtu fulani ukikubali unachokifanya.

Namba 4:Kala Jeremiah- Wana ndoto

Ni kati ya nyimbo za Hip hop zilizoweza kumkutanisha mtoto mmoja aliepotea kwa mama yake na akaja kuonekana katika video hii jambo ambalo mama mzazi wa kijana huyo ikabidi amatafute Kala na hatimaye kumpata kijana wake. Wana ndoto inafaa kwa rika zote hasa kwa wale wanaojiona wanamapungufu lakini wamesahauliwa kuwa wana uwezo wakufanya jambo fulani.

Namba 5: Iko sawa Muzik- John Stephen Akhwari

Hili ni kundi la muziki linalotokea Arusha, linaundwa na Budz107 na Justin Cukaz ambaye ni producer wa muziki na Director pia. Ngoma hiyo ya John Stephen Akhwari, inanatokana na jina la mwanariadha huyo kutokea Tanzania aliyeenda katika mashindano ya olympic marathon mwaka 1968 nchini Mexico.
Katika mbio za kilomita 42 wakati John Stephen Akhwari amefika km 19 alianguka chini na kupata majeraha ya goti pamoja na kisigino ambapo aliumia na ikawa vigumu kuendelea kukimbia lakini yeye aliamini amekwenda kuiwakilisha nchi yake na akajikongoja hadi kumaliza mbio hizo, jambo amabalo watu walimshangilia sanas

Na Laila Sued

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents