Fahamu

Fahamu :Sehemu hizi za kutembea siku ya Sikukuu ukiwa Dar es Salaam

Kama upo ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam na umesha maliza pilika piliaka za kuweza kula katika Siku kuu ya Eid basi si haba kuweza kutafuta sehemu ya kupumzika na kufurahia siku hiyo pamoja na familia.

Hizi ni sehemu tano kwa Mkoa huo kuweza kuzitembelea paoja na famila.

1. Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni

Kama unapenda historia na unataka kujua zaidi kuhusu historia na utamaduni ya Tanzania, Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni ndio sehemu ya kutembelea. Makumbusho haya yanaonyesha mengi yakiwemo urithi wa kikabili, ufundi wa kitamaduni, vifaa vya muziki, sanaa ya kitanzania, historia ya kikolony na ya kisiasa na zaidi.

2. Kijiji cha Makumbusho – Kijitonyama

Makumbusho, kama inavyoitwa kwa kifupi, itakupeleka ndani ya Tanzania vijijini kwa kuonyesha tofauti ya vijiji vya Tanzania, kabila kwa kabila. Wanabaadhi za nyumba za kiasili ambazo unaruhusiwa kuingia. Kwa kifupi, Kijiji cha Makumbusho itakupa uzoefu wa utamaduni ya Tanzania.

3. Kisiwa ya Mbudya

Kama unataka kupumzika fukweni ukiwa Dar, Kisiwa ya Mbudya ndio pakwenda. Njia rahisi kufika mbudya ni kwa kupanda boti kutoka Jangwani Sea Breeze Resort iliyopo Mbezi Beach, na kawaida hakujai. Kwa hiyo, unaweza kutulia hapo kwa raha zako.

4. Coco Beach

Fukwe ya Coco ambayo ipo Msasani Peninsula sehemu hii ni maarufu pia kwa kuza vitu kama mishkaki na muhogo wa kuchoma. Fukwe ya Coco inapendwa sana na familia au marafiki wa aina zote.

5. Kijiji ya Wamakonde, Mwenge

Kama unatafuta sanaa, nguo, viatu, begi, vifaa vya jikoni, chochote kile, utavikuta kwenye Kijiji ya Wamakonde. Eneo lote limetengwa kwa ajili ya kukuza sanaa ya kitanzania. Zaidi ya hapo, mara nyingi wauzaji ndio wasanii wenyewe kwa hiyo wanaweza wakakutengezea kitu chakipekee.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents