Michezo

Fahamu takwimu za Liverpool klabu bingwa na alichosema, Jurgen Klopp

Liverpool ilionyesha mchezo mzuri katika historia yake baada ya kutoka nyuma na kuilaza Barcelona kwa jumla ya magoli 4-3

Image result for klopp

Baada ya kupoteza kwa magoli 3-0 katika uwanja wa Nou camp , Liverpool ililipiza kisasi wakati Divock Origi alipoiweka kifua mbele timu hiyo.

Georginio Wijnaldum alifunga magoli mawili katika dakika mbili ili kusawazisha.

Mara baada ya ushindi huo Klopp ameshindwa kuamini kilichofanywa na vijana wake akisema hata hafamu waliwezaje ” Mechi yote kwa jumla ilikuwa zaidi’ , alisema Klopp. Kushinda ni vigumu lakini bila jibu , sijui waliwezaje kufanikiwa”.

Origi baadaye alifunga goli lake la pili na la nne kwa upande wa Liverpool kutokana na kona iliopigwa kwa haraka ili kukamilisha ushindi mkubwa.

Liverpooll sasa huenda ikacheza dhidi ya Ajax ama Tottenham katika fainali ya kombe la vilabu bingwa mjini Madrid mnamo tarehe mosi mwezi Juni.

Ilikuwa mazingaombwe kwa Barcelona ambao walicharazwa 3-0 na Roma katika mkondo wa pili wa robo fainali ya kombe hilo mwaka uliopita kutokana na goli la ugenini , baada ya kushinda mkondo wa kwanza 4-1.

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp alishindwa kujizuia baada ya kushuhudia kikosi chake kikitoka nyuma na kuwalaza mabingwa hao wa La Liga .

Lakini kwa Liverpool ilikuwa kumbukumbu nyengine ya matokeo mazuri ya Ulaya ambayo yanafananishwa na ushindi wao dhidi ya AC Milan katika fainali ya 2005 na ushindi wao wa 4-3 dhidi ya Borussia Dortmund katika uwanja wa Anfield miaka mitatu iliopita.

Ni mara ya kwanza tangu 1986-wakati Barcelona ilipoilaza Gothenburg katika kombe la Ulaya-ambapo timu ilitoka nyuma kwa magoli matatu kushinda nusu fainali ya michuano hiyo.

Baada ya magoli hayo manne mashabiki wa nyumbani walisimama wakiishabikia timu yao katika dakika za mwisho huku wachezaji wa Barca walioshangazwa wakishindwa kujibu mashambulizi ya Liverpool.

Kipenga cha mwisho kilipopulizwa kilileta sherehe kubwa ndani ya uwanja na katija maeneo ya mashabiki.

Liverpool imefanikiwa kutoka nyuma na kushinda katika siku za nyuma , hususana wakati waliposhinda taji lao la tano mjini Istanbul lakini ushindi huu dhidi ya barcelona ndio mkuybwa katika historia ya klkabu hiyo wanapojiandaa kucheza dhidi katika fainali mji Madrid.

Sio mara ya kwanza kwa Barcelona kuadhibiwa kwa kiwango hiki, baada ya kufungwa 3-0 na Roma katika robo fainali mwaka uliopita baada ya kushinda mkondo wa kwanza 4-1 hivyobasi wataendelea kusubiri kutinga fainali tangu 2015.

Walichezewa katika kila safu na ijapokuwa walipata fursa kadhaa hawawezi kudai kwamba walihitaji kushinda.

Kulikuwa na kipindi kifupi katika kipindi cha kwanza , wakati mabingwa hao wa La Liga walipoamka na kuanza mchezo wao mzuri na katika kipindi cha dakika tano kipa Allison alimnyima Messi na Phillipe Coutinho huku Jordi Alba akilazimika kutoa pasi wakati ambapo alikuwa amesalia na kipa huyo kucheka na wavu.

Messi ambaye alikuwa mchezaji mwenye kasi kubwa wiki moja iliopita alishindwa kutawala hususan katika kipindi cha pili wakati magoli ya Wijnaldum yalioposawazisha.

Mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez pia alipotea huku mchango wake ukionekana wakati ambapo alizomwa mara kwa mara na mashabiki ambao walizoea kumuabudu.

Alikuwa na fursa nzuri katika kipindi cha pili , wakati Messi alipompatia pasi nzuri huku Liverpool ikiwa 1-0 usiku huo lakini Allison alikuwa macho na hiyo ndio iliokuwa nafasi ya mwisho wageni hao kutekeleza tishio lolote.

Georginio Wijnaldum alifunga goli la Pili

Takwimu za Liverpool kombe la klabu bingwa

  • Liverpool imefanikiwa kutinga fainali ya tisa katika klabu bingwa Ulaya huku Real Madrid wakifika mara 11 nayo Bayern wakitinga mara 10.
  • Ndio timu ya kwanza katika ligi ya Uingereza kutinga fainali mara mbili mfululizo tangu Manchester United mwaka 2008 na 2009.
  • Hii ni mara ya nne kwa timu kutoka nyuma ikiwa 0-3 katika mkondo wa kwanza wa klabu bingwa ili kusonga mbele. Barcelona pia iliondolewa kama hivyo mwaka uliopita dhidi ya Roma.
  • Barcelona kufikia sasa wameondolewa katika michuano mitatu kati ya minne ya nusu fainali ya klabu bingwa iliopita.
  • Mabingwa hao wa La Liga walishindwa kwa magoli mengi dhidi ya klabu ya Uingereza katika mashindano yote ya Ulaya.
  • Beki wa kulia Trent-Alexander Arnold ametoa usaidizi mara 14 katika mashindano yote msimu huu , zaidi ya wachezaji wengine wa Liverpool.
  • Divock Origi alifunga magoli yake ya kwanza ya klabu bingwa na hivyobasi kuwa mchezaji tofauti wa 50 wa Liverpool kuifungia Liverpool.
  • Georginio Wijnaldum ni mchezaji wa kwanza wa Liverpool kufunga magoli mawili kama mchezaji wa ziada tangu Ryan Babel dhidi ya Besikitas 2007.
  • Pia ni mchezaji wa kwanza wa ziada kufunga katika mechi moja dhidi ya Barcelona katika michuano hiyo.
  • Lionel Messi alijaribu kufunga magoli matano mbali na kutengeneza pasi tatu katika mshambulizi yote ya Barcelona dhidi ya Liverpool katika mechi hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents