Tupo Nawe

FAHAMU: Timu 7 zilizoungana na Simba SC kufuzu hatua ya robo fainali klabu bingwa Afrika

Jana klabu ya Simba imefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali kwa kuichakaza AS Vita ya DR Congo goli 2-1, na kuungana na klabu nyingine 7 kutoka mataifa mbali mbali.

Klabu ambazo zimeungana na Simba SC ni Espérance Tunis (Tunisia), CS Constantine (Algeria), TP Mazembe (DR Congo), Horoya AC (Guinea), Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini), Wydad Athletic Club (Morocco) na Al Ahly ya Misri.

Droo ya robo fainali itatangazwa wiki lijalo Machi 20, 2019 ambapo michezo itaanza mwezi wa Aprili mwaka huu.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW