Habari

Fahamu toleo jipya la Tecno Camon X linalokuja kuteka soko la simu janja duniani (+Video)

Mitandao ya kijamii kama Instagram, Facebook, Snapchat na Twitter imekuwa ikiwafanya watumiaji wa simu za mikononi nchini Tanzania na duniani kuhakikisha wanakuwa na simu kali zenye uwezo wa kupiga picha kali na kuziposti muda huo huo bila hata kuzifanyia editing.

Picha zilizopigwa na Tecno Camon X

Kampuni ya simu ya Tecno imejua nini watumiaji wa simu za mkononi wanataka na kuamua kutengeneza simu zenye uwezo mkubwa wa kuchukua picha na hilo limeonekana kwenye matoleo yake yote ya awali.

Sasa habari njema ni kwamba kampuni hiyo ya simu janja duniani inayokua kwa kasi zaidi imetangaza ujio wa toleo jipya la Camon X yenye uwezo mkubwa zaidi katika kuchukua picha.

Camon X itakuwa na sifa nyingi kulinganisha na matoleo mengine ambapo ujazo wa ndani wa simu hiyo unatarajiwa kuwa ni 32/64 gb na RAM 3/4 huku uwezo wa kamera ya nyuma yenye kamera mbili zenye ukubwa wa Megapixel 12+20.

Toleo hilo linakuwa la pili kwa mwaka 2018 hii ni baada ya Tecno kutoa toleo lao jipya la Camon CM ambalo lilikuwa la kwanza kuwa na Display ya uwiano wa 18:9 .

Simu hiyo itakuwa ni toleo la kwanza kwa Tecno kuwa na kamera mbili za nyuma hivyo itakuwa na uwezo wa kuchukua picha kwenye mazingira yoyote kwa ubora wa hali ya juu.

Kwa mujibu wa mtandao wa Tech Weez umeeleza kuwa simu hiyo ni maalumu kwa watu wanaopenda kupiga picha ingawaje ina imeboreshwa kwenye kila idara ukilinganisha na matoleo mengine ya Tecno.

Mtandao huo umesema kuwa kamera za simu hiyo zitakuwa na uwezo wa ku-zoom hadi megapixel 60 kitu ambacho kitakufanya mtumiaji kupiga picha za mbali na kuonekana vizuri.

Kwa upande wa kamera ya mbele kwa wale watu wanaopenda picha za selfie, Camon X inakuja na kamera iliyoboreshwa zaidi na itakuwa na flash kwa ajili ya kutumia sehemu zenye mwanga hafifu.

Sifa nyingine za simu hiyo ni kwamba itakuwa na utambuzi wa sura (Face ID) na fingerprint hii ni kwa ajili ya usalama wa simu yako.

Kwa upande wa umbo la simu hiyo itakuwa nyembamba na yenye kushikika kiurahisi ikiwa na display ya ukubwa wa kioo chenye inchi 6 .

Mara nyingi watu wengi wamekuwa wakiboreka kwa simu zao kupata joto wakati wakifungua programu zaidi ya moja, lakini kwa Camon X hilo halitatokea kabisa kwani simu hiyo imetengenezwa na mfumo wa kupunguza joto automatic pindi inavyopata joto ( Cooling system) hivyo bila shaka kwa watumiaji wanaoishi maeneo yenye joto kama Dar es salaam hii itakuwa simu yako ya ndoto.

Simu hiyo inatarajiwa kuzinduliwa April 5 mwaka huu nchini Nigeria na baadaye duniani kote.

Makala hii imeandaliwa na Godfrey Mgallah na Yassin Ngitu.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents