DStv Inogilee!

FAHAMU: Uki-google neno mpumbavu ‘Idiot’ picha ya kwanza itakayotokea kwenye mtandao huo ni ya Rais maarufu zaidi duniani

FAHAMU: Uki-google neno mpumbavu 'Idiot' picha ya kwanza itakayotokea ni ya kiongozi maarufu zaidi duniani

Unaweza ukashangaa kwa hili lakini ndio ukweli kuwa endapo utaandika kwenye search engine ya google neno ‘IDIOT’ lenye maana ya neno Mpumbavu basi picha ya kwanza itakayotokea kwenye kipengele cha ‘images’ ni ya kiongozi mkubwa Duniani.

 

Na kiongozi huyo sio mwingine bali ni Rais wa Marekani, Donald Trump hii ni kutokana na mitandao mingi kuanza kuandika matokeo hayo siku ya jana.

screen-shot-2018-07-16-at-08.17.00-0.png

Hata hivyo, sio Rais Trump peke yake kwenye orodha hiyo bali yupo pia Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte ambaye wiki mbili zilizopita alisikika akimkashifu Mungu kwa kumtolea lugha za kebehi.

Mwingine mtu maarufu ni Rapa Kanye West naye pia ametokea kwenye picha za juu baada ya ku-google neno Idiot yaani mpumbavu.

Wiki iliyopita Rais akiwa kwenye ziara yake nchini Uingereza alishindwa kutofautisha kati ya U.K (United Kingdom), Britain na England kitu ambacho kilizua mijadala mikubwa kwenye mitandao ya kijamii.

Hata hivyo mpaka sasa bado Google mpaka sasa hawajaeleza kwanini uki-google neno ‘idiot’ inatokea picha ya Rais Donald Trump.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW