Mitindo

Fahamu urembo wa tatoo

Katika ulimwengu wa mitindo ata sanaa ya michoro utumika kurembesha kitu fulani ndio maana unakuta nyumba imepambwa na urembo wa picha za michoro, hata kwenye mwili ya binadamu wengine upendelea kuchora michoro tofauti kama tatoo.

Baadhi ya mastaa bongo wamechora tatoo zaidi ya moja na wengine wakidai ukichora tatu lazima uchore nyingine na nyingine kwani inakufanya uwe unatamani tamani, tatoo ina michoro tofauti tofauti miaka ya 90 wengi walichora nanga pamoja na fuvu, miaka ilivyozidi kwenda kukaja mchoro wa kappa, na sasa michoro ya maua na majina imeonekana kupendwa zaidi.


Wanaume wengi upendelea kuchora michoro ya majina na picha kama za siura za wazazi wao ama watoto wao au maandishi ya kitu furani.

Kwa upande wa wamawake upendelea picha za maua hasa ua rose, upendelea nembo kama kopa(love) ama kitu fulani pia kuandika majina ama maandishi ya kitu fulani.

Tatoo uvutia zaidi kwa mtu mwenye rangi angavu yani mweupe kuliko mwenye rangi nyeusi kwani haitaonekana vizuri. Ila zingatia kuwa kabla ya kuchora tatoo unaona  na wataalau wa masuala ya ngozi iliusipate madhara kama kuvimba mwili ama kutokwa na vipele.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents