Michezo

Fahamu uwezo wa mwanasoka bora wa mwaka duniani kwa wanawake (Video)

Tumeshazoea kuyasikia majina makubwa kwenye mpira wa miguu kama Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kwa upande wa wanaume, je umeshawahi kulisikia jina la Lieke Martens kwa upande wa wanawake?

Basi huyu ndio mshindi wa tuzo ya mchezaji bora kwa upande wa wanawake mwaka huu ambaye ametangazwa jana mjini London. Mchezaji huyu ana umri wa miaka 24 na anachezea timu ya taifa ya Uholanzi na klabu ya soka ya wanawake ya Barcelona.

Mchezaji huyu amejiunga na Barca Julai 12 ya mwaka huu akitokea FC Rosengård ya Sweden, lakini amewahi kucheza katika ligi mbalimbali ikiwemo Ubelgiji, Ujerumani, Sweden na sasa ligi ya wanawake ya Hispania.

Lieke ambaye anavaa jezi namba 22 Barca na jezi namba 11 timu ya taifa, amebarikiwa kuwa na kiwango kikubwa cha soka huku akionyesha uwezo wake wa kucheza vizuri katika nafasi ya kiungo na mshambuliaji.

Mpaka sasa Lieke amefanikiwa kuifungia Barcelona mabao mawili katika mechi sita ambazo ameshachena na timu ya taifa ya Uholanzi ameshaifungia mabao zaidi ya 31 katika mechi 75 alizocheza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents