Fahamu

Fahamu :Vyuo vikuu bora duniani kwa mwaka 2017

Watu wengi huangalia vyuo vyenye majina na wingi wa wanafunzi wakiamini ni vyuo vitakavyo kuwa bora ama kuwawezesha kufauru katika masomo yao.

Kwa mujibu wa Taasisi ya Times Higher Education imebainisha vyuo vidogo bora duniani, ambapo walifanya utafiti kupiti wanafunzi wanosoma katika vyuo hivyo.

1.Chuo cha California Institute of Technology (Caltech)- Marekani

Chuo kikuu cha Caltech kilichopo nchini Marekani kimekuwa katika nafasi ya kwanza na kina mazingira mazuri ya kimasomo kwa miaka kadhaa mfululizo kina wanafunzi 2,000.Kwa mujibu wa wanataaluma nafasi ya walimu na wanafunzi wa chache inaleta fursa ya majadiliano kwa upana katika chuo hicho.Caltech kinafundisha masomo katika taaluma ya sayansi na teknolijia ambayo yanafundishwa na maprofesa nguli.

2.Chuo cha Sayansi na Tekinolojia (POSTECH)- Korea Kusini

Chuo cha POSTECH kilianzishwa mwaka 1986, kwa kila mwaka huwachukua wanafunzi 320 katika njia maalumu ya usaili. Wanafunzi wa chuo hicho wanasifia madarasa yake madogo na kina maprofesa wanawajua kwa majina kila mwanafunzi.

3.École Polytechnique -Ufaransa

Chuo cha École Polytechnique kipo katika ubora wake hivi karibuni kimezindua masomo ya shahada ya uzamivu katika baadhi ya masomo na pia mwaka huu kilianzisha masomo ya taaluma ya hesabu.

4.Scuola Normale Superiore di Pisa – Italia

Hiki ni chuo kingine cha itwacho Scuola Normale Superiore di Pisa ni kidogo na kina wanafunzi 545, kinatoa kozi mbalimbali katika masuala ya sayansi.Lengo kuu la chuo lilikuwa na kutafuta uhusiano kati ya wanafunzi wa sayansi na masomo ya maliasili watu.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents