Fahamu

FAHAMU: Wanawake 7 matajiri zaidi duniani kwa mwaka 2019 na jinsi walivyoingiza mkwanja

Kwa mujibu wa jarida la Forbes hii ndio orodha ya wanawake 7 matajiri zaidi duniani kwa mwaka 2019.

1. Françoise Bettencourt-Meyers

Francoise Bettencourt-Meyers in 2011

Thamani yake Dola bilioni 49.3, ni mtu wa 15 tajiri zaidi duniani kwa mujibu wa jarida la Fobes.

Yeye ni nani?

Ni mfaransa mrithi wa kampuni ya vipodozi ya L’Oréal ambaye anamiliki 33% ya kampuni hiyo na familia yake.

Mwanamke huyo wa miaka 65 alirithi mali utajiri huo kutoka kwa mama yake Liliane Bettencourt, aliefariki dunia mwezi Septemba mwaka 2017 akiwa na miaka 94.

Wawili hao walizozana kwa miaka kumi kuhusiana na usimamizi wa kampuni hiyo hadi wakafikishana mahakamani mwaka 2007.

Bi Bettencourt-Meyers aliwasilisha kesi mahakamani akihoji kuwa washirika wa karbi na mama yake walikuwa wakimlaghai licha ya hali yake mbaya ya kiafya.

Lakini waliafikiana miaka kadhaa kabla ya kifo cha mama yake.

2. Alice Walton

Alice Walton

Thamani yake : Dola biloni 44.4, thamani ambayo inamuorodhesha katika nafasi ya 17 ya watu tajiri zaidi duniani.

Yeye ni nani?

Mwanamke huyo aliye na umri wa miaka 69 ni binti wa kipekee wa mwanzilishi wa duka kubwa zaidi la jumla nchini Marekani,Sam Walton.

Hata hivyo tofauti na ndugu zake wawili wa kiume, alijitenga na biashara ya familia na kujiingiza katika biashara ya sanaa na kuwa mwenyekiti wa makavazi ya sanaa nchini Marekani inayofahamika kama Crystal Bridges Museum iliyo na makao yake mjini Bentonville, Arkansas.

3. MacKenzie Bezos

Jeff and MacKenzie

UTAJIRI WAKE: Ni karibu na dola bilioni 35.6 -ndio thamani yake katika kampuni ya Amazon pekee, lakini thamani yake halisi inatarajiwa kuwa juu zaidi ya hiyo.

Yeye ni nani?

Mama huyo wa miaka 48 amezaa watoto wanne na mwasisi wa mtandao wa Amazon, ambaye alimuoa mwaka 1993 walipokua wakifanya kazi pamoja katika hazina ya hedge, na baada mwaka jana wakatengana jambo ambalo limesababisha wagawane hisa kwenye kampuni ya Amazon.

Mkaazi huyo wa California alikua miongoni mwa wafanyikazi wa kwanza wa kampuni ya Amazon, na awali alifanya kazi kama mhasibu.

4) Jacqueline Mars

Jacqueline Mars

Thamani yakeNi dolaola bilioni 23.9 – ni mtu wa 33 tajiri zaidi duniani kabla ya enzi ya MacKenzie Bezos ( sawa na wanawake wengine katika orodha inayofuata hapo chini).

Yeye ni nani?

Mwanamama huyu wa miaka 79 ni mzaliwa wa tatu katika familia ya Mars, kampuni kubwa zaidi ya uokaji dunia ambayo alianzishwa na babu yake Frank mwaka 1911.

Alifanya kazi katika kampuni ya familia yake kwa karibu miaka 20 nakuwa katika bodi ya usimamizi wake hadi mwaka 2016.

5. Yan Huiyan

Image result for Yan Huiyan

Thamani yake: Dola bilioni 22.1, thamani ambayo inamfanya kuwa mwanamke tajiri zaidi nchini China na mtu wa 42 tajiri zaidi duniani.

Yeye ni nani?

Mwanadada huyu mwenye umri wa miaka 37 anamiliki hisa katika kampuni kubwa ya ujenzi nchini China inayofahamika kama Coutry Garden Holdings, ambayo inaongoza katika biashara ya sekta ya ujenzi China.

Kwa mujibu wa utafiti Country Garden, ilikua kampuni kubwa zaidi ya ujenzi kote duniani mwaka 2016.

Yan Huiyan, amerithi 57% ya hisa ya kampuni hiyo kutoka kwa baba yake.

6. Susanne Klatten

Susanne Klatten

Thamani yake Ni dola bilioni 21, ambayo inamweka katika nafasi ya 46 ya watu tajiri zaidi duniani.

Yeye ni nani?

Ni mtu wa pili kutoka barani Ulaya katika orodha ya watu tajiri zaidi duniani.

Mwanamke huyu raia wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 56 ana mchanagnyiko wa magari na makampuni ya dawa.

Alirithi 50% ya kampuni ya kutengeneza dawa ya Altana AG wakati wazazi wake walipofariki, huku ndugu yake wa kiume akimiliki 50% ya kampuni ya uundaji magari ya BMW.

Hata hivyo ameifanya kampuni ya Altana kuwa yake binafsi baada ya kununua hisa zote za kampuni zingine kubwa.

7. Laurene Powell Jobs

Laurene Powell Jobs

Thamani yakeNi dola bilioni 18.6, thamani inayomfanya kuwa mtu wa 54 tajiri zaidi duniani.

Yeye ni nani?

Ni mjane wa mwanzilishi wa kampuni kubwa ya teknolojia ya Marekani Apple, Steve Jobs.

Familia yake ilimiliki takriban dola bilioni 20bn katika kampuni za Apple na Disney wakati mume wake alipofariki dunia.

Tangu wakati huo, Bi.Laurene mwenye umri wa miaka 55 aliendelea mbele na kukuza utajiri wake kwa kuwekeza sehemu ya fedha zake katika sekta ya habari, kwa kumili hisa nyingi katika jarida la Atlantic , pamoja na uchapishaji wa wa majarida ya Mother Jones na ProPublica.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents