Fahamu

FAHAMU: Wimbo wa muziki wa ‘Gloomy Sunday’ unaodaiwa kusababisha vifo vya watu 100 duniani kote (video)

Wimbo wa Gloomy Sunday wenye maana ya Jumapili ya Huzuni unatajwa kuwa ndio wimbo wa muziki uliosababisha vifo vya watu mia 100 duniani kote, hii ni kwa mujibu wa jarida la How Stuff Works.

Wimbo huo ulitungwa na kuimbwa na mwanamuziki kutoka Hungary aitwaye, Rezso Seress mnamo mwaka 1933.

Katika wimbo huo, Reszo alitunga maneno ya wimbo huo na kupiga mwenyewe ala ya huzuni ya wimbo huo, baada ya kuachwa na mpenzi wake.

Kitendo cha kuachwa na mwanamke huyo, kilimfanya apatwe na msongo wa mawazo na huzuni. Jambo lililomfanya apate wazo la kutunga mashairi ya wimbo huo na baadae kutunga wimbo huo.

Wimbo huo unaotia huzuni na upweke, aliuimba akiwa na huzuni za mtu anayelalamika kuvunjwa moyo na mpenzi wake aliyempenda.

Kwenye moja ya mashairi yake amefananisha kitendo cha kuachwa, kuwa ni sawa na kufiwa na mpenzi aliyekuwa anampenda kwa dhati.

Mwanzoni mwa miaka ya 1935, wimbo huo ulionekana kuwa wimbo wa kawaida wa huzuni, lakini baadae matukio ya watu kujiua baada ya kuusikiliza mara nyingi wimbo huo, yalianza kuripotiwa.

Na watu wengi waliojiua waliacha ujumbe, kwamba wamejiua baada ya kusikiliza wimbo huo.

Jambo ambalo miaka miwili baadae (1937), Serikali ya nchini Hungary iliupiga marufuku wimbo huo kutumika kwa namna yoyote ile.

Kutokana na umaarufu wa wimbo huo barani Ulaya, baadhi ya wasanii waliutafsiri wimbo huo na kuuimba kwa kiingereza jambo ambalo lilizidi kuonmgeza maafa kwa mataifa yanayotumia lugha hiyo.

Imeelezwa kuwa Mjini Paris nchini Ufaransa watu zaidi ya wanne walijiua mnamo mwaka 1938.

Tukio la kwanza ni wanaume wawili walijipiga risasi baada ya kusikiliza wimbo huo uliokuwa ukipigwa na bendi live kwenye Bar, na wawili ni wanafunzi walikunywa sumu na kuacha ujumbe uliosomeka maneno mawili ‘Gloomy Sunday’ na mmoja aliyejiua alikuwa ni fundi viatu yeye alijichoma na sindano tumboni huku radio yake ikiwa na kanda ya wimbo huo.

Baada ya kuenea kwa matukio hayo, mwaka 1940, toleo la Kiingereza la wimbo huo lilipigwa marufuku nchini humo. Baada ya idadi ya waliokuwa wakijiua kuzidi kuongezeka lakini Marekani na sehemu nyingine duniani wimbo huo uliendelea kupigwa.

Imeelezwa kuwa baada ya wimbo huo kumpatia mafanikio makubwa duniani kote, Rezso aliamua kumtafuta mwanamke aliyemkimbia miaka hiyo na kusababisha atunge wimbo huo.

Lengo la kumtafuta lilikuwa ni kujaribu kumbembeleza ili warudiane, kwani kwa kipindi hicho alikuwa na maisha mazuri. Hata hivyo, katika hali ya kustaajabisha, alipofika mahali alipokuwa akiishi mwanamke huyo, alikuta watu wamejaa, baadaye ikabainika kwamba mwanamke huyo alijiua kwa kunywa sumu chumbani kwake na kuandika ujumbe wenye maneno mawili ‘Gloomy Sunday’.

Hata hivyo, Rezso naye mwenyewe mwaka 1968, aliamua kujiua kwa kujirusha ghorofani kupitia dirisha la chumba alichokuwa akiishi, mjini Budapest. Na kuacha ujumbe uliosomeka “Nimeamua kujiua kutokana na wimbo wangu kuua watu wengi pasipo kukusudia kama ujumbe wa wimbo wangu ungegarimu maisha ya watu wengi”.

Wimbo wa ‘GLOOMY SUNDAY’ bado umefungiwa na mataifa karibia yote barani Ulaya, ila kwa bara la Afrika na Amerika bado unapigwa kwenye vyombo vya habari.

Visa vingi vya watu kujiua vimetokea kwa wingi katika nchi za Hungary, Ufaransa, Italia na Uingereza .

Fahamu zaidi kuhusu wimbo huo kwa kuusikiliza na kusoma mashairi yake hapa chini.


Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents