Fahamu

Fahamu zaidi kuhusu mtoto wa miaka 7 aliyeng’olewa zaidi ya meno 525 kinywani mwake, huko India

Fahamu zaidi kuhusu mtoto wa miaka 7 aliyeng'olewa zaidi ya meno 525 kinywani mwake, huko India

Mtoto wa miaka saba ambaye alikuwa akilalamikia kuumwa na taya yake amepatikana na meno 526 ndani ya mdomo wake kulingana na hospitali moja nchini India ambapo alikuwa akifanyiwa matibabu. Mtoto huyo alikuwa amelazwa mwezi uliopita katika mji wa kusini wa Chennai kutokana na uvimbe na maumivu karibu na meno yake ya nyuma katika taya yake ya chini ya kulia.

Kulingana na mtandao wa Zee News, wakati madaktari walipomfanyia ukaguzi katika kinywa chake waligundua kijifuko katika taya yake ya chini kilichojaa meno yasio ya kawaida.

Kulingana na afisa mkuu wa maswala ya vinywa katika hospitali ya meno na Taasisi ya mafunzo ya Seveetha, huku upasuaji wa kutoa meno hayo ukifanyika mwezi uliopita , madaktari walihitaji muda ili kuchunguza kila jino kabla ya kuthibitisha matokeo yao.

“kijifuko hicho kilikuwa na uzito wa gramu 200, tulikitoa polepole”.

Mtandao huo unasema kwamba wazazi wake waligundua uvimbe huo wakati alipokua na umri wa miaka mitatu .Lakini hawakujali sana kwa kuwa uvimbe huo haukuwa mkubwa.

”Lakini baadaye wakati uvimbe huo ulipoanza kuongezeka ,wazazi hao walimleta mvulana huyo kwa hospitali yetu”, alisema Profesa P.Senthilnathan wa idara ya maswala ya vinywa na upasuaji siku ya Jumatano.

Vipande vya meno 526

Anasema picha iliopigwa kwa kutumia miyale ya X-ray ilibaini meno mengi yaliowafanya madaktari hao kumfanyia upasuaji unasema mtandao wa Zee News.

Ijapokuwa kulikuwa na vipande vidogovidogo, madaktari wanasema kuwa vilikuwa na ishara ya meno. Ilichukua takriban saa tano kwa madaktari hao kutoa meno hayo madogo kutoka katika kifuko hicho.

Kwa mujibu wa BBC. ”Kijana huyo alirudi katika hali yake ya kawaida siku tatu baada ya upasuaji” , alisema Pratibha Ramani Profesa na kiongozi wa idara ya vinywa katika hospitali hiyo.

Dr Pratibha Ramani, ambaye alihusika katika upasuaji huo aliambia gazeti la Times nchini India kwamba meno hayo yalikuwa na ukubwa tofauti uliotofautiana kati ya milimita 0.1 hadi milimita. .

Kulingana na madaktari hao hicho ndicho kisa cha kwanza duniani kwa mtu mmoja kupatikana na meno mengi madogo.

Kulingana na daktari Senthilnathan ugunduzi huo ulionyesha kwamba kuna umuhimu kufanyiwa ukaguzi wa kinywa wa mapema iwezekanavyo.

Picha ya meno ya X-Ray

Alisema kwamba ijapokuwa hamasa ya magonjwa ya vinywa inaimarika nchini humo, aliongezea kwamba katika sehemu za mashambani bado kuna tatizo.

”Zamani masawala kama ukosefu wa madaktari wa meno, ukosefu wa elimu, ufukara ulimaanisha kwamba hakuna hamasa ya kutosha. Lakini matatizo haya bado yapo, Unaweza kuwaona watu katika miji wana hamasa ya kutosha lakini watu wanaoishi katika maeneo ya mashambani hawana elimu ama hata uwezo wa kuwa na afya nzuri ya vinywa vyao”.

”Kwa kisa cha Ravindrath. Kila kitu kimekuwa sawa- mvulana huyo sasa ana meno 21 yenye afya” , alisema Dkt.Dr. Senthilnathan.

Kulikuwa na kisa kama hicho mjini Mumbai 2014 ambapo meno 232 yalitolewa kutoka kwa mdomo wa kijana.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents