Afya

Faida na hasara za unywaji wa kahawa na chai

Chai au kahawa ni vinywaji vinavyopendwa na watu wengi wa jamii zote duniani kama kiamsho kwa asubuhi au jioni. Pamoja na kuwa ni vinywaji ambavyo vimezoeleka sana kwa matumizi ya kawaida katika jamii nyingi bado vinywaji hivi vinaweza kuwa na faida na hasara zake kiafya.

Faida za Kahawa na Chai:

1. Kahawa au chai inaweza kukuongezea nguvu mwilini

Kikombe cha chai na kahawa kinaweza kukufanya usijisikie mchovu na kukuongezea nguvu mwilini.

Hii ni kwa sababu ndani yake kuna kuna kichangamsho (stimulant) kiitwacho kafeina.
Tafiti nyingi zinathibitisha kaffeina huimarisha kazi kadhaa za ubongo. Kazi hizo ni pamoja na zile zinahusiana na masuala ya kumbukumbu, tabia, nguvu, uharaka wa kujibu mambo nk.

2. Husaidia kuchoma mafuta mwilini

Kama ulikuwa hujuwi kaffeina ni kiungo mhimu kwenye dawa nyingi za kupunguza uzito au mafuta mwilini za viwandani ingawa wakati mwingine inaweza isitwaje kwenye vifungashio vya hizo dawa.

Kaffeina ni moja ya viinilishe vya asili ambavyo vimethibitishwa kuwa vinasaidia kuchoma mafuta mwilini. Tafiti kadhaa zinaonyesha kaffeina inaweza kuuongezea nguvu mfumo wa mmeng;enyo wa chakula kwa asilimia 3 mpaka 11.

3. Kuna viinilishe kadhaa vizuri kwenye chai na kahawa

Kahawa au chai ya rangi ni zaidi ya yale maji meusi. Kuna viinilishe kadhaa vizuri kwa mwili wa binadamu. Viinilishe hivyo ni pamoja na vitamini B5, manganizi, potasiamu, magnesiamu nk

4. Kafeina inaweza kukuepusha kisukari aina ya pili

Kisukari aina ya pili ni janga la kidunia na ni ugonjwa unatesa watu zaidi ya milioni 300 dunia nzima. Kwa kiasi fulani wanywaji wa chai na kahawa wanapata kinga ya kutokupata kisukari aina hii ya pili. Tafiti zinaonyesha kuwa watu wanaokunywa chai ya rangi na kahawa wana asilimia mpaka 67 za kutokupata kisukari aina hii.

5. Kaffeina inaweza kuwa mlinzi kwa Ini

Ini ni ogani ya pekee sana mwilini na ina kazi nyingi mhimu sana kwa mwili. Magonjwa kadhaa yanaathiri ini moja kwa moja kama vile hepatitis A, B na C, magonjwa ya mafuta katika ini na mengine kadhaa. Mengi ya magonjwa haya hupelekea makovu kadhaa katika ini hali ijulikanayo kwa kitaalamu kama ‘cirrhosis’. Watu wanaokunywa chai au kahawa wana asilimia mpaka 80 za kutokupata magonjwa mbalimbali ya ini.

6. Kaffeina inaweza kukuondolea msongo wa mawazo

Msongo wa mawazo au mfadhaiko ni ugonjwa hatari ambao unaweza kukupunguzia ubora wa maisha yako. Ni hali ya kawaida kwa miaka ya sasa huku ikiathiri karibu asilimia 4 ya watu. Katika utafiti mmoja uliofanywa na chuo kikuu cha Harvard Marekani mwaka 2011 iligundulika wanawake wanaokunywa kahawa na chai vikombe viwili mpaka vitatu kwa siku walikuwa na kiasi kidogo sana cha uwezekano wa kupatwa na mifadhaiko (stress).

Madhara ya Chai na Kahawa Kiafya:

Pamoja na faida kadhaa hapo juu za matumizi ya kahawa na chai bado kuna hasara kadhaa za kutumia vinywaji hivi. Kwenye chai na kahawa kuna kitu kinaitwa kafeina.

1. Kafeina ni madawa ya kulevya katika kundi la madawa yanayoamsha mwili

Hii ndiyo sababu kwa mtu aliyezoea kunywa chai hii kila siku au kahawa, siku asipokunywa kichwa humuuma, ni kwa sababu amekuwa mtegemezi au teja wa kafeina. Kafeina ni kiungo mhimu karibu katika soda zote zenye rangi nyeusi; Coca-cola, Pepsi, Sayona nyeusi, Azam cola na kadharika. Kafeina huongezwa pia katika Red bull, Malta na katika baadhi ya dawa za kupunguza maumivu mwilini.

2. Kafeina ni kikojoshi (diuretics).

Kafeina ni dawa ya kukufanya ukojowe. Ukinywa kikombe kimoja cha kinywaji chenye kafeina yaani chai au kahawa, basi muda si mrefu utaenda kukojoa vikombe viwili. Kwa sababu kafeina ni taka isiyotakiwa mwilini, mwili utafanya kila uwezalo ikibidi ujikamuwe wenyewe kupata maji ya ziada kuweza kuitoa kafeina hii uliyoinywa kwa kisingizio cha chai, kahawa au soda.

3. Kafeina husababisha KANSA.

Seli ndani ya mwili lazima zibaki katika kiasi kidogo cha alkalini kutoka 7.2 mpaka 7.4, wakati 7.0 ni ya kati au husemwa sifuri katika kipimo cha PH (potential hydrogen). Chini ya 7.0 ni asidi na juu ya 7.0 ni alkalini.
Kafeina yenyewe ni asidi, hivyo ikiwa mtu anafanya chai au kahawa ndivyo vinywaji vyake vya kila siku basi mtu huyo lazima atakuja kupatwa na kansa katika siku za usoni kwakuwa seli za kansa huishi katika hali ya uasidi pekee na kafeina ndimo mazingira mazuri ya kuishi asidi.

Jarida moja la afya la Uingereza, ‘The British Medical Journal Lancet’, limeripoti uhusiano mkubwa uliopo baina ya utumiaji wa kahawa na kansa ya kibofu cha mkojo na kupungua kwa uzarishwaji wa mkojo.

4. Kaffeina huchangia upotevu wa madini na vitamini mhimu mwilini.

Kafeina ambayo ni kikojoshi, huyalazimisha maji kukimbia nje ya mwili kwa haraka na kuziacha seli bila muda wa kutosha kuyatumia maji hayo, maji yanapokimbia kwa haraka nje ya mwili huyakimbiza pia madini mhimu nje ya miili yetu.

5. Uchovu sugu.

Wapenzi wengi wa chai ya rangi na kahawa mara nyingi wanapojisikia uchovu hukimbilia kikombe cha kahawa au chai.Kaffeina iliyomo katika chai au kahawa huenda kuiamsha na kuitumia nguvu iliyokuwa imehifadhiwa na mwili kwa ajili ya matendo ya dharura na kukuacha wewe ukiwa huna nguvu ya ziada kwa ajili ya kazi za dharura, matokeo yake ni mwili unakuwa upo katika hali ya msukosuko muda wote.

Kituo cha Sayansi kwa maslahi ya umma (Center for Science in Public Interest) kimewashauri kinamama wajawazito kukaa mbali na kafeina kwa kuwa tafiti zimeonesha kwamba kiasi cha kafeina kilichomo kwenye vikombe 4 vya kahawa kwa siku kinaweza kusababisha matatizo wakati wa kujifungua kama yalivyoonwa katika majaribio kwa wanyama.

Madhara ya chai ya rangi na kahawa mwilini ni mengi sana na tatizo moja litapelekea lingine na orodha inakuwa haiishi.

Namna ya kuepuka kaffeina kwenye kahawa na chai:

Kwa upande wa kahawa ikiwa una tatizo lolote la kiafya na ungehitaji kupata uponyaji wa haraka basi ningekushauri uamuwe tu kuacha kutumia kwanza kahawa.

Au ikiwa umeanza kuonyesha dalili za matatizo haya nimeyaainisha kama matokeo ya kutumia kahawa basi ni vema ukachukuwa uamuzi wa kuacha kuitumia. Wakati mwingine inaweza isiwe kazi rahisi sababu ina kawaida ya kukupa uteja wa kuitumia kila siku lakini penye nia pana njia na hakuna lisilowezekana.

Kwa upande wa chai ya rangi kama unapenda kunywa chai asubuhi, badala ya kutumia majani hayo ya chai meusi, wewe chemsha maji yako ya chai kama kawaida na unaweza kutumia vifuatavyo kukamilisha chai yako; unaweza kutumia tangawizi na kumbuka pia tangawizi ni dawa ya zaidi ya magonjwa 72 mwilini.

Unaweza pia kuweka mdalasini, mchaichai, kukamulia ndimu, pia unaweza kutumia mchanganyiko wa viungo vingi vya chai (spiced tea).

Chanzo: Fadhili Paulo

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents