Technology

Faida ya Samsung yaongezeka kwa asilimia 50 licha ya sakata la simu za Galaxy Note 7 kulipuka

By  | 

October mwaka jana, watumiaji wa Samsung duniani kote waliripoti kuwa simu zao za Galaxy Note 7 zilikuwa zinashika moto na kuifanya kampuni hiyo izirudishe kiwandani simu zote.

Licha ya kikwazo hicho ambayo kimedaiwa kimeigharimu kampuni hiyo dola bilioni 3, faida ya Samsung iliongezeka zaidi mwaka jana.

Kampuni hiyo imesema faida ya robo ya mwisho ya mwaka jana ilikuwa ni zaidi ya asilimia 50, na kiwango kikubwa zaidi katika miaka mitatu.

Wachambuzi wanasema faida nyingi zimetokana na biashara ya semiconductor.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments