Michezo

Fainali ya NBA: LeBron James ‘hajawahi kumuacha mtu salama’

Usiyempenda kaja. Timu ya mchezo wa kikapu ya Cleveland Cavaliers imeonekana imeanza kukurupuka katika usingizi mzito waliolala mwanzoni kwenye mchezo wa fainali ya nne wa ligi ya kikapu ya Marekani dhidi ya Golden State Warriors.

Katika mchezo huo uliochezwa alfajiri ya kuamkia leo, Cavaliers wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani Quicken Loans Arena, wameshinda jumla ya vikapu 137 dhidi ya 116 vya Worriors. Kwa hatua hiyo Golden wanaongoza kwa kushinda jumla ya michezo 3-1 ya fainali hizo.

https://youtu.be/SKDtcZiiJzY

Wakati huo huo, nyota LeBron James kutoka Cleveland amejitengeneza rekodi nyingine ya mashindano hayo akiwa mchezaji watatu kwa kufunga magoli mengi katika fainali za NBA, tayari amefunga alama 1,176 akiwa nyumba ya Jerry West (1679) na Kareem Abdul-Jabbar (1317) wote waliwahi kuichezea Los Angeles Lakers.

Mashabiki wengi wanaendelea kuusubiri kwa hamu mchezo wa fainali ya tano ambao utachezwa alfajiri ya siku ya Jumanne katika uwanja wa Oracle Arena.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents