Burudani

Faiza Ally achoshwa na jeshi la polisi nchini ‘natamani ningekua mzungu’

Muigizaji wa Filamu nchini Tanzania, Faiza Ally amefunguka kuwa kama angekuwa na uwezo wa kubadili utaifa wake basi angefanya hivyo na kuchangua nchi za Ulaya, kwani anaona maisha ya Tanzania yanamuwia magumu kwa upande wa uhuru wa mtu binafsi na haki za kibinadamu.

Faiza Ally

Faiza amesema hayo baada ya kudai kuwa jeshi la polisi nchini limeshikilia simu yake ya mkononi kwa miezi mitatu sasa tangu aposti picha yake akiwa leba kwenye mitandao ya kijamii.

Kama kuna siku nimeamka na maumivu makali ni leo , leo ni siku ambayo natamani ningekua mzungu niishi katika nchi zenye haki za kibinaadamu , maana kuna wkt unahisi unaonewa kwenye nchi yako! Huu ni mwezi wa 3 toka police wachukue simu yangu I phone 7+ yenye thamani ya shilingi M.3 , inaniuma sana , kila wiki naripoti police sasa nimeanza kupewa wiki mbili, mbili, kisa ni picha yangu ya leba wao wana hesabu kama phonographs,“ameandika Faiza Ally kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kwa upande mwingine mrembo huyo amesema juzi Jumamosi alilitaarifu jeshi hilo kuwa amechoka kuripoti polisi akiwataka ajue mwisho ni lini lakini polisi walimwambia aendelee kuripoti hadi mwanasheria atakaporudisha jalada la uchunguzi.

Juzi nimwaambia nimechoka jamani naombeni sasa nijue kuripoti huku mwisho lini? wanasema hawajui mpaka mwanasheria arudishe Jalada, nimewaomba nimuone mwanasheria wamesema siruhusiwi wao ndio wanatakiwa wafatilie ndio wa nipe majibu,“ameandika Faiza Ally.

Soma na Hii – Faiza Ally baada ya kuposti picha akiwa leba ‘Nimepongezwa sana’ 

Mwishoni mwa mwaka jana mrembo Faiza aliposti picha kwenye mitandao ya kijamii akiwa leba, picha ambayo ilizua taharuki kwenye jamii na ndiyo iliyopelekea simu yake kushukuliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi.

SOMA WARAKA ALIOANDIKA FAIZA ALLY KUHUSU MALALAMIKO YAKE JUU YA JESHI LA POLISI

Kama kuna siku nimeamka na maumivu makali ni leo , leo ni siku ambayo natamani ningekua mzungu niishi katika nchi zenye haki za kibinaadamu , maana kuna wkt unahisi unaonewa kwenye nchi yako! Huu ni mwezi wa 3 toka police wachukue simu yangu I phone 7+ yenye thamani ya shilingi M.3 , inaniuma sana , kila wiki naripoti police.

Sasa nimeanza kupewa wiki mbili, mbili, kisa ni picha yangu ya leba wao wana hesabu kama phonographs, juzi nimwaambia nimechoka jamani naombeni sasa nijue kuripoti huku mwisho lini? wanasema hawajui mpaka mwanasheria arudishe Jalada, nimewaomba nimuone mwanasheria wamesema siruhusiwi wao ndio wanatakiwa wafatilie ndio wa nipe majibu, nimwaambia changamoto ninazo pitia kuhusu kukosa simu, kwanza mm nimfanya biashara kwenye mitandao contact zangu zote , mails , number za cm , picha zipo humo napata wakati mgumu kwenye kazi zangu.

Naombeni simu yangu, na kumbukumbu zangu na wanangu muhimu sana zote zipo humu maisha yangu bila hiyo simu ni magumu mno, mm ni mama wa watoto wawili, ugali wangu, ada ya mwanangu , kodi ya nyumba na duka zote nategemea kupitia humu , kiufupi cm yangu ndio maisha yangu jamani naombeni mnirudishie , ndio kwanza nimepewa wiki mbili zingine na sina mategemeo, nikiuliza simu yangu ya nn wanasema wana ichunguza , najiuliza mnaichunguza nini mpaka leo miezi mitatu sielewi, jamani sijawahi kuwa muuza bangi wala Unga wala jambazi au muhujumu wa serekali au mtuhumiwa wa aina yoyote mnaichunguza nini???😭😭😭😭

Nimewaza mpaka nimetamani ningekua na mabwana kama sita hivi mmoja aninunulie simu niendelee na maisha yangu, najitahidi nisimame bila mabwana lkn mwisho wa siku wanawake tukizidiwa hakuna namna ! Sasa hivi sio sawa ni kama mnarudisha juhudi za maisha yangu nyuma ! Naombeni mtoe hukumu yangu nimechoka kuzungushwa, kama mnanipeleka mahakamani nipelekeni, nijue moja .mimi jamani siwezi kuacha au kusamehe simu ya millioni 3 jamani hali ya maisha ni ngumu na lzm niwe na simu yenye viwango kutokana na kazi yangu , sasa nalazimika kulipia camera kwa ajili ya kushuti video ya matangazo ya biashara zangu ktkna na nilio nayo haina uwezo, na lzm kupata garama zaidi SEREKALI NAOMBA MSAMAHA KWA KOSA LANGU , MAISHA YANGU YAMESIMAMA😭

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents