Burudani

Fally Ipupa anusurika kifo kwenye ajali ya gari huko Kinshasa

Mwanamuziki maarufu wa Congo Fally Ipupa, wiki hii amenusurika kifo baada ya gari aliyokuwa akisafiria kupata ajali huko mji mkuu wa DRC, Kinshasa.

fally2

Mwimbaji huyo kipenzi cha kinadada alitoka salama bila kuumia, huku taarifa zingine zikidai kuwa abiria mwenzake msichana ambaye hajafahamika alikimbizwa hospitali. Inasemekana kuwa Fally alikuwa akitokea studio wakati ajali hiyo ilipotokea Jumanne usiku.

Fally_Ipupa_Car_Crash_1
Hii ni gari aliyopata nayo ajali Fally Ipupa

Fally_Ipupa_Car_Crash_2

Baada ya ajali hiyo kumekuwepo na habari za uvumi mtandaoni kuwa mwanamuziki huyo ameumia sana, huku zingine zikidai kuwa amepoteza maisha kutokana na ajali hiyo, lakini Fally aliutumia ukurasa wake wa facebook kuweka sawa taarifa hizo.

“Mimi ni mzima…ni gari tu ndio imeharibika, Asante Mungu. Asanteni kwa meseji zenu.” Ameandika Fally.

Source: Standard Digital

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents