Habari

Familia ya mkosoaji wa Serikali ya Rais Paul Kagame yakamatwa na polisi

Kiongozi wa upinzani na mkosoaji mkubwa wa Serikali nchini Rwanda, Bi. Diane Rwigara na familia yake (Mama yake na Mdogo wake wa kike) wamekatwa na polisi jana wakiwa nyumbani kwao mjini Kigali.

Bi. Diane Rwigara

Polisi wamesema kuwa familia hiyo ilifanya makosa ya ulaghai kwa kukwepa kulipa kodi huku ikidai kuwa familia hiyo imekuwa tishio kwa usalama wa taifa hilo hivyo watashikiliwa mpaka uchunguzi utakapokamilika.

Bi. Rwigara ni mwanamke pekee nchini Rwanda aliyejitosa kwenye mbio za kugombea urais kwenye uchaguzi mkuu nchini humo uliofanyika mwezi Agosti, ambapo jina lake lilikatwa na Tume ya Uchaguzi baada ya picha zake za utupu kuvujishwa na watu wasiojulikana mtandaoni.

SOMA ZAIDI – Picha za utupu za mgombea urais Rwanda zavuja mtandaoni

Taarifa kutoka kwenye gazeti la IGIHE zinasema kuwa Bi Rwigara mbali na tuhuma za ukwepaji kodi pia anatuhumiwa kutumia nyaraka za serikali za watu waliokwisha fariki kwenye kipindi cha uchaguzi mkuu vikiwemo vitambulisho vya wapiga kura.

Bi. Diane amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Rwanda huku akimtuhumu Rais wa nchi hiyo, Paul Kagame kubana Demokrasia.

Hii inakuwa ni mara ya pili kwa familia hiyo ya bilionea wa zamani wa Rwanda,  Assinapol Rwigara kukamatwa kwani mwezi uliopita walikamatwa na kuachiwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents