Habari

Familia ya ‘MO’ yatangaza zawadi ya Sh Bilioni moja kwa atakayetoa taarifa zitakazosaidia kupatikana kwa  Mo Dewji

Familia ya mfanyabiasha Mohammed Dewji maarufu kama ‘MO’ hii leo imetangaza kiasi cha shilingi bilioni moja kwa yoyote atakaye saidia kufanikisha kupatakana kwake baada ya kutekwa majira ya saa 11: 35 mpaka saa 11: 40 tarehe 11 Oktoba  2018 Colosseum Hotel Mtaa wa Haile Selasie Oysterbay Dar es salaam kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mwanafamilia huyo aliyezungumza na vyombo vya habari.

Katika mkutano huo na vyombo vya habari familia hiyo imetaja namba ambazo zitatumika katika kutolea taarifa zitakazowezesha kupatika kwake ambazo ni 0755 030 014 /0755 030 014 na 0717 20 84 78 na 0784 78 32 28.

”Tunapenda kutoa taarifa kwa vyombo vya habari ambazo zinaweza kutusaidia, kutangaza katika kutekwa kwa mtoto wao mpendwa ndugu Mohammed Dewji ‘MO’ Mtendaji mkuu wa makampuni ya MeTL Group mnamo alfajiri ya saa 11: 35 mpaka 11: 40 tarehe 11 Oktoba  2018 Colosseum Hotel Mtaa wa Haile Selasie Oysterbay Dar es salaam.”

Hata hivyo familia hiyo imeishukuru Serikali, viongozi wadini na waandishi wa habari kwa kutoa ushirikiano wao katika jambo hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents