Familia ya Oscar Pistorius kuifikisha mahakamani filamu ya ‘Oscar Pistorius: Blade Runner Killer’

Familia ya mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius imedai kuwa itawasilisha mahakamani zuio la filamu inayohusu maisha ya ndugu yao na jinsi alivyomuuwa mpenzi wake Reeva Steenkamp mwaka 2013.

Filamu hiyo iliyopewa jina la ‘Oscar Pistorius: Blade Runner Killer’ inatarajiwa kutoka Novemba mwaka huu.

Familia ya Pistorius imesema kuwa filamu hiyo imeonyesha kitu ambacho sio cha kweli kilichotokea siku ya tukio hilo. “Filamu hiyo sio kweli ya kile kilichotokea siku ya janga hili ni jaribio la baadae la jambo hilo. Tutachukua hatua za kisheria,” imesema familia hiyo.

Mwezi Julai mwaka jana Oscar alihukumiwa kifungo cha miaka sita jela kwa kosa hilo la mauaji ya mpenzi wake.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW