Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Familia yakatwa mapanga na watu wasiojulikana

Watu wawili ambao wametambulika kama mume na mke wakazi wa kitongoji cha Kidogue wilayani Mkalama wameuawa papo hapo kwa kuchabangwa na mapanga huku wengine wakijeruhiwa kwenye maeneo mbalimbali ya miili yao na watu wasiojulikana.

Wanandoa hao waliotambulika kwa majina ya Kija Kitundu (53) na mkewe Mwajuma Ramadhan (59) waliuawa na watu hao Desemba 10, 2017 saa sita usiku wakiwa wamelala nyumbani kwao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Debora Magiligimba amethibitisha taarifa hizo ambapo amesema watoto wa wanandoa hao, Ramadhani (14) na Namagalu (12), wamepelekwa hospitalini kwa matibabu baada ya kujeruhiwa vibaya katika tukio hilo.

Magiligimba amesema kuwa siku ya tukio wauaji hao ambao hawajajulikana mpaka sasa walitumia ngazi kupanda juu ya paa la nyumba ya kisha kuingia chumbani kwa wanandoa hao na kuwacharanga mapanga.

Chanzo:Mwananchi

Leave a comment

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW