HabariUncategorized

Fatuma Karume atema cheche: Kuwa mwanaharakati sio dhambi, hakuna kitu kinanikera kama…

Rais wa Chama Cha Wanasheria Tanzania, TLS Bi Fatuma Karume aliyechukua mamlaka baada ya aliyekuwa Rais wa Chama hicho, Tundu Lissu kushindwa kuendelea na uongozi kutokana na kupigwa risasi na watu wasiofahamika, amefunguka mambo mengi kuhusu utawala wa sheria nchini Tanzania, katiba mpya pamoja namna baadhi ya watu wanavyowachukulia vibaya wanaharakati.

Rais wa Chama Cha Wanasheria Tanzania, TLS Bi Fatuma Karume.

Akiongea na Arnold Kayanda wa kituo cha BBC mapema leo, Fatuma amesema hadhani kama serikali ina mahusiano mabaya na chama hicho cha mawakili.

“Mwaka jana serikali ilikuwa imesema TSL itatufutwa, tumefanya nini hatujui, tumewakosea nini hatujui,” alisema Fatuma “Mimi ningesema serikali ina wasiwasi na TLS, wanahisi kwamba iko pale kama wapingani wao. Kazi ya TLS ni pale serikali haifuati sheria na taratibu pamoja na utawala wa sheria TLS itasema,” alisema mtoto huyo wa Rais mstaafu wa Zanzibar.

Aliongeza, “Mimi nadhani serikali inahisi tukisema, tunakuwa kama wapinzani, sisi tutaendelea kukosoa na hiyo serikali isiogope. Kukosolewa ni kitu kizuri kwa sababu ukikosolewa unaweza ukajirekebisha na tutawakosoa kwenye mambo ya sheria,”

Mwanasheria huyo amedai kwa sasa TSL inapigania haki za watu, haki za binadamu pamoja na kuhakikisha sheria zilizotungwa na Bunge zinasimamiwa.

Katika hatua nyingine Fatuma amedai TSL kwa sasa haina ajenda ya katiba mpya lakini yeye binafsi anaona kuna umuhimu wa kubadilisha katiba ya mwaka 1977 kwa madai wananchi wamenyimwa nguvu nyingi kwa nchi yao.

“Rais anateua kila mtu nchi hii, inamaana kwamba ukiwa mteuzi una haki pia ya kufukuza, una haki ya kuteua wakuu wa mikoa, unateua wakuu wa wilaya, unateua wakuu wa polisi, una haki ya kuteua majaji, power yote ya wananchi imechukuliwa na imewekwa kwenye mkono wa mtu mmoja, kama watanzania hatuwezi kukubali kuendelea kuwa na urais wa kiufalme,” alisema Fatuma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents