Habari

FBI yasema mshambuliaji wa Ohio alikuwa na itikadi ya ghasia

Maafisa wa uchunguzi nchini Marekani wamesema mtu aliyewauwa kwa kuwapiga risasi watu tisa katika jimbo la Ohio nchini humo amekuwa akijihusisha na itikadi ya ghasia.

Image result for FBI TO ATTACK TO OHIO REPOTED

Shirika la Upelelezi la FBI lilianzisha uchunguzi wake kuhusiana na nia ya mwanaume huyo aliyekuwa na umri wa miaka 24 na limesema kuna mashaka iwapo shambulizi hilo lilichochewa na ubaguzi wa rangi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la DW, Todd Wickerham, wakala wa FBI huko Cincinnati ametoa kauli hiyo licha ya kuwa sita kati ya watu tisa waliouwawa na mshambuliaji huyo walikuwa weusi.

Shambulizi hilo lilitokea saa chache baada ya shambulizi jengine jimboni Texas katika duka la jumla la Walmat mjini El Paso. Kwa jumla watu 31 waliuwawa katika mashambulizi yote mawili yaliyohusisha ufyatuaji wa risasi.

Mshambuliaji wa Ohio aliuawa na Polisi. Rais Donald Trump ambaye anashutumiwa kuhamasisha chuki kupitia kauli zake kali, anatarajiwa kuizuru miji miwili iliyokumbwa na mashambulizi baadaye leo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents