Michezo

FC Barcelona watoa ‘gundu’ lililodumu miaka 11 La Liga

Klabu ya Barcelona jana imefanikiwa kupata ushindi wa goli 4-2 kwenye mchezo wa ligi kuu nchini humo (La Liga) dhidi ya Real Sociedad.

Magoli ya Barcelona yamefungwa na Luis Suarez x2, Lionel Messi na Paulinho huku magoli mawili ya Sociedad yakifungwa na Willian Jose na Juanmi.

Ushindi huo wa Barcelona unakuwa wa kwanza tangu mwaka 2007, klabu hiyo ilipopata ushindi wa mchezo wa Ligi kwenye Uwanja wa Estadio Anoeta.

Hata hivyo, gundu hilo la Barcelona kukosa matokeo kwenye dimba la Estadio Anoeta lingeendelea kama sio juhudi binafsi za Luis Suarez na Lionel Messi kwani hadi mapumziko tayari Barca walikuwa wameshapigwa goli 2-1.

Tazama msimamo wa La Liga kwa sasa baada ya mechi za wikiendi iliyopita.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents