Federer awapa somo wachezaji tennis dhidi ya Novak Djokovic

Mchezaji tennis namba moja kwa viwango vya ubora duniani, Roger Federer amewataka wenzake kumuheshimu Msebia, Novak Djokovic licha ya kutolewa katika hatua za mapema za michuano ya Indian Wells .

Mchezaji tennis raia wa Sebia, Novak Djokovic 

Federer ambaye ni raia wa Uswisi na bingwa wa michuano ya wazi ya Australia mwaka 2017 amesema, Djokovic ataendelea kuimarika siku hadi siku na kurejea katika kiwango chake baada ya kuwa nje ya uwanja kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 kwa takribani miezi sita toka kupoteza pambano lake mwaka uliyopita la Wimbledon na baadaye dhidi ya Hyeon Chung hatua ya raundi ya nne ya Australian Open.

Djokovic ametolewa katika hatua za mapema raundi ya pili ya Indian Wells dhidi ya Mjapani, Taro Daniel kwa seti 7-6, (7-3),4-6,6-1.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW