Michezo

Fedha siokigezo cha kumsajili Messi – Arguero

Wakati mkataba wa mchezaji bora wa dunia anaekipiga katika timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi unaelekea ukingoni, nyota wa Man City, Sergio Aguero amesesm ni vigumu kwa timu yake kumsajili mkali huyo wa soka.

 

Aguero ambaye anacheza timu moja ya taifa na Messi amekiri kuwepo kwa ugumu wa kuinasa saini ya nyota huyo kwakuwa mchezaji huyo ni nembo ya klabu ya Barcelona.

“Napenda kuwa na Lionel Messi hapa Manchester City lakini itakuwa vigumu kwakuwa yeye ni nembo ya klabu hivyo hawezi kuondoka Barcelona.” Amesema Aguero.

Aguero haamini kama kunatumaini la Messi kujiunga na City, hata kama fedha si tatizo kwa klabu yake.

“Fedha siyo tatizo lakini nafikiri Messi ni kama Cristiano Ronaldo wachezaji hawa ni alama katika klabu zao na hivyo inawawia vigumu kuzihama,”

 

Aguero hakuwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Argentina ambacho kimecheza wiki hii kutafuta tiketi ya kufuzu kombe la dunia baada ya kupata ajali ya gari huko Amsterdam mwishoni mwa mwezi Septemba iliyomsababishia kuvunjika kwa mbavu zake.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, ameonyesha huwenda akawa katika kikosi kitakachoikabili timu ya Stoke City siku ya Jumamosi huku akitoa ufafanuzi juu ya lawama alizopewa ya kukutwa na ajali nchini Uholanzi wakati klabu yake ikiwa inajiandaa na mchezo wa ligi.

Amesea sababu ya kwenda Jijini Amsterdam ilikuwa ni kwasababu alikuwa katika siku zake za mapumziko, “Wakati wachezaji wa Manchester City wanapopata siku za mapumziko wengi hupenda kwenda London, wengine Itali na wengine nchini Hispania. Mimi nilikuwa na bahati ya kufahamiana na wakala wa Maluma ‘muimbaji wa Colombia’ amenialika na nikaamua kwenda kutumia mapumziko yangu huko na wakati nafikwa na ajali nilikuwa njiani naelekea uwanja wa ndege tayari kurudi.”

Straika huyo wa Man City, Aguero mpaka sasa hana uhakika kama atacheza mchezo wa siku ya Jumamosio licha ya kuwa leo ameanza mazoezi binafsi na kesho akitarajia kujumuika na kikosi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents