Soka saa 24!

Felix Simbu aandika ujumbe mzito ‘Kwenye mafanikio tufurahi na kwenye shida tushikamane’

Baada ya mwanariaza wa Tanzania, Alphonce Felix Simbu kupoteza kwenye mashindano ya New York city marathon, amewaomba radhi Watanzania kwa matokeo hayo.

Simbu ameomba radhi kupitia mtandao wake wa kijamii wa Face book.

Habari Tanzania. Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru sana Watanzani wote na wasio Watanzani kwa maombi yao juu ya mashindano ya New York city marathon ingawa mimi nimeshindwa kufanya vizuri na pia nimeshindwa kumaliza kabisa.

Naomba niwatie moyo tusikate tamaa kwani bado kuna mashindano mengi mbele tuendee kumwomba mungu ili atusaidie wachezaji wa Kitanzania tuendee kuiwakilisha nchi yetu vyema katika mashindano mbali mbali yajayo.
Tukumbuke kuwa kila jambo linachangamoto zake.

Na napenda kuwaambia sio kila mara itakuwa wewe kuna wakati wa kupanda na wa kushuka pia. Kwenye mafanikio tufurahi na kwenye shida tushikamane.
Nawashukuru sana na Mungu awabariki. Amen.

Mwanariadha huyo ameshindwa kukimbia katikati ya mashindano baada ya misuli ya paja kumbana.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW