Habari

Felix Tshisekedi atangazwa rasmi na Mahakama kuwa Rais mteule wa DR Congo

Mahakama ya Kikatiba ya nchini DR Congo, jana Jumamosi Januari 19, 2018 imemtangaza rasmi Felix Tshisekedi kama Rais aliyechaguliwa na wananchi kwenye uchaguzi uliofanyika Desemba 30 mwaka jana.

Image result for felix tshisekedi

Katika uamuzi uliosubiriwa kwa hamu na raia wa nchi hiyo, Mahakama hiyo ilitupilia mbali ombi la mgombea mwingine wa upinzani, Martin Fayulu ambaye alikuwa anadai kwamba matokeo ya awali yaliyotolewa na tume ya uchaguzi ya DRC, CENI, hayakuwa halali.

Katika uamuzi wao, majaji wa mahakama hiyo walisema kuwa Fayulu hakutoa ushahidi wa kutosha kuonyesha kwamba kura zake ziliibiwa.

Kufuatia uamuzi wa mahakama hiyo, ambayo ndiyo yenye kauli ya mwisho kuhusu masuala ya uchaguzi, sasa Tshisekedi anaweza kuapishwa muda wowote.

Matokeo yaliyotangazwa na tume ya Uchaguzi huo yalimuonesha, Tshisekedi akiwa amepata kura milioni 7, sawa na asilimia 38 ya kura zote zilizopigwa.

Martin Fayulu aliyekuwa anapinga matokeo alipata kura milioni 6.3, huku Emmanuel Ramazani Shadary wa muungano wa vyama tawala – na ambaye alikuwa anungwa mkono na rais wa sasa, Jeseph Kabila, akiwa katika nafasi ya 3 kwa kuzoa kura milioni 4.3 .

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents