Burudani

Fella anogewa na taarab

Video_Sharo_fella

Mwanamuziki Saidi Fella ama ukipenda unaweza kumwita Mkubwa Fella au Mkubwa na Wanawe, kati ya leo ama kesho anatarajia kuachia ngoma yake mpya ya Midomo imewashuka katika miondoko ya pwani maarufu kama Taarabu.


Katika miondoko hiyo, Fella  inaonekana amekolewa na staili hiyo hasa baada ya kufanya vizuri katika wimbo wake wa kwanza aliomshirikisha Isha Ramadhani ama Isha Mashauzi ‘Jike la Simba’.

Fella amesema katika wimbo huo amemshirikisha mwanamuziki anayechipukia katika kundi la Mkubwa na wanawe band Hassan Kumbi , huku kukiwa na mkono wa Producer Suresh, toka studio ya Poteza Record.

Aidha Fella ameongeza kwa kusema, zaidi ya nyimbo hizo za taarabu lakini sasa anakuja na albamu kamili.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents