Burudani

Fella atambulisha kundi jipya kutoka Mkubwa na Wanawe, ni SALAMU TMK

Meneja mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Said Fella kabla mwaka 2015 haujaisha ametambulisha kundi jipya kutoka kwenye kituo chake cha Mkubwa na Wanawe.

fella3

Kundi hilo lenye vijana saba linaitwa Salamu TMK na tayari wameachia wimbo wao mpya ‘Nafsi’ pamoja na video yake.

“Vijana wetu wapya kutoka mkubwa na wanawe vijana wanaitwa #SALLAM TMK awa vijana wako saba tunawatoa mtaani wanaitaji kufika mjini na kupata nguvu binafsi ya kuthubutu kupata kununua mkate aya wadau ngoma ya vijana SALLAM TMK inaitwa NAFSI tunaomba sapot ya vijana kwa uzuri wametoka mikoa mitano. Mbeya vijana wailing, zanzibar mmoja,songea mmoja, kigoma kasuru mmoja na dar vijana wawili. Aya wadau nguvu zinaitajika” aliandika Fella kupitia Instagram.

Kundi hilo limefata baada ya Yamoto Band ambao pia wako chini yake, kufanya vizuri mwaka 2015, ikiwa ni pamoja na kuanza kupata show za nje ya nchi.

Itazame hapa kazi ya kwanza ya Salamu TMK ‘Nafsi’

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents