Habari

Fema Radio Show: Dar es Salaam hupokea vijana laki moja kila mwaka kutoka mikoani

Jiji la Dar es Salaam hupokea vijana zaidi ya laki moja kutoka mikoani kila mwaka wanaokuja kutafuta maisha. Takwimu hizo ni kwa mujibu wa mdau wa masuala ya vijana, Gadi Kalugendo aliyekuwa akizungumza wiki hii kwenye kipindi cha Fema Radio Show kinachoandaliwa na shirika la Femina HIP.

1

Msimu mpya wa kipindi hicho unaangalia suala la vijana wengi kukimbilia jijini Dar es Salaam.

Kalugendo amesema idadi hiyo ni ya vijana kati ya miaka 15 mpaka miaka 35 ambayo ni nje na idadi nzima ya watu wanaohamia Dar es Salaam ambayo ni kubwa zaidi.

“Ukijaribu kuangalia kwa idadi hiyo ya vijana wanaoingia Dar es Salaam, kila mwaka vijana laki moja ni idadi kubwa sana. Dar es Salaam sasa hivi ina vijana wengi kuliko umri ambao umeshazidi ujana,” anasema Kalugendo.

“Na tukitaka tufanikiwe ni kuhakikisha kwamba tusiwazue wale vijana kuja huku,hatuna jinsi lazima waje hii ndio Dar es Salaam lakini lazima tuwaandalie mazingira ambayo yatawasababisha waje Dar es Salaam na waweze kukidhi haja ya mahitaji yao yanayowasababisha waje.”

Kalugendo amesema kupitia shughuli za vijana ameweza kugundua kuwa wengi wa vijana wanaotumia madawa ya kulevya wamezaliwa jijini Dar es Salaam lakini asilimia 30 ya vijana wanaotumia madawa hayo wametokea mikoani.

“Wanatoka kule na malengo kwamba wanakuja Dar es Salaam kuna shughuli za kufavya, wakifika huku wanakuta hakuna shughuli za kufanya, anaingia kwenye bangi kidogo kidogo anakwenda kwenye madawa ya kulevya,” anaeleza Kalugendo.

Fema Radio Show huruka kila Jumatatu saa 2:45 usiku RFA na Jumanne saa 3 kupitia TBC FM. Kama ulikosa sikiliza hapa.

Part 1

Part 2

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents