HabariUncategorized

Femina Hip wakabidhi zawadi kwa washindi wa insha ya ‘Stori Yangu Kuhusu Hedhi’

Shirika lisilokuwa la kiserikali la Femina Hip Jumamosi hii limefanya hafla ya utoaji zawadi kwa washindi 10 walioshinda katika shindano la kuandika insha (Essay) ya ‘STORI YANGU KUHUSU HEDHI’ kwa wanafunzi wa shule za sekondari hapa nchini.

Katika utoaji wa zawadi hizo ulihuzuliwa na mgeni rasmi Sauda Simba, Wawakilishi wa timu ya nguvu ya binti wakiongozwa na Lydia Charles, Badru Juma, Walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari Chang’ombe na Zinga, Amabilis Batamula, Tunu Yongolo na wengine.

Wanafunzi 10 kutoka shule tofauti tofauti wakiwemo wasichana watano na wavulana watano walitangazwa kushinda katika shindano hilo na kukabidhiwa zawadi zao.

Katika insha hiyo vijana walitakiwa kuandika maneno yasiyopungua 600 na kuzidi 1000 huku pia wakitakiwa kuzingatia vigezo vitano vilivyowekwa ikiwemo ubunifu, kuendana na mada husika, hisia, mtiririko, na matumizi ya lugha.

Wanafunzi wa shule ya Chang’ombe wametajwa kuongoza katika shindano hilo kwa kutoa washindi watatu, lakini pia wametajwa kuwa ndio shule ambayo wanafunzi wake wengi waliandika Insha hinzo na kuzituma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents