Afya

Fernanda Martinez: Nina mwaka wa pili sijawahi kula chakula chochote kutokana na ugonjwa ninaougua

“Nini kitakachokea usipokula chochote?” Fernanda Martinez amekuwa akiulizwa swali hilo kila wakati anapojumuika na marafiki zake katika mitandao ya kijamii. Lakini amekuwa akiwajibu kwa kuwapa maelezo kuhusu hali isiyokuwa ya kawaida katika mfumo wake wa jeni, ambao umemfanya ashindwe “kula chakula”.

Msichana huyo raia wa Brazil mwenye umri wa miaka 22- anakabiliwa na hali inayofahamika kwa kimombo kama Ehlers-Danlos syndromes (EDS), ambayo husababisha, kuzaana kwa seli zisizokuwa za kawaida mwilini- na ambazo huathiri mfumo wa utumbo.

Kuna aina tofauti ya EDS na karibu mmoja kati ya watu 5,000 duniani hukabiliwa na hali hiy , kwa mujibu wa shirika linalotoa hamasisho kuhusu ugonjwa wa Ehlers-Danlos.

Fernanda amekuwa akiishi kwa kulishwa chakula kupitia mipira tangu mwaka 2018 kwa sababu utumbu wake hauwezi tena kusaga chakula vyema.

Licha ya kukabiliwa na hali hiyo, amekuwa akiishi na saratani ya koo, ambayo imewaathiri jamaa zake kwa muda.

Lakini Fernanda ameamua kuufahamisha ulimwengu kuhusu hali yake kwa kuiangazia katika mitandao ya kijamii.

Ruka Instagram ujumbe, 1

Mwisho wa Instagram ujumbe, 1

Changamoto kubwa inayomkabili Fernanda ni kushindwa kula wala kunywa kitu chochote, kwasababu hawezi kufanya hivyo.

Njia pekee inayowezesha mwili wake kupata virutubisho muhimu anavyohitaji ni kupitia njia ya sindano inayodungwa kwenye mshipa.

“Ni sawa na kusaga chakula kilicho na virutubisho vyote kisha kinachunjwa na kuingizwa mwilini mwake moja kwa moja kupitia sindano anayodungwa kwenye mshipa,” anaelezea mtaalamu wa lishe bora Pamela Richa, ambaye huandamana na Fernanda anapoenda kwa matibabu.

Fernanda imekuwa akiwaelezea maelfu ya watu wanaomfuatilia katika mitandao ya kijamii jinsi mfumo huo wa lishe unavyofanya kazi, iwe ni kupitia kwa akaunti yake binafsi ama mradi wa unaoangazia jinsi ya kuishi na ugonjwa huo isiokuwa ya kawaida .

Maelezo yake yamepata umaarufu. Video zake za kuwapa motisha wale wanaokabiliwa na hali kama yake zimetazamwa na watu zaidi ya miolioni moja katika mtandao wa kijamii wa TikTok.

Video za Fernanda katika mtandao wa TikTok huvutia watazamaji zaidi ya milioni moja
,Video za Fernanda katika mtandao wa TikTok huvutia watazamaji zaidi ya milioni moja

“Maswali ya watu hayanivunji moyo kwasababu napata msaada kutoka kwa watu ambao wamebadili mtazamo wao kuhusu jinsi wanavyoshughulikia mambo,” Fernanda aliiambia BBC.

Tatizo la Fernanda lilianzaje?

“Nilipokuwa mtoto mdogo, Nilionesha dalili kwamba kuna kitu ambacho hakipo sawa mwili ni mwangu,” anaeleza.

“Nilikuwa mtoto aliyekuwa na maumivu miguuni na mikononi. Nilizaliwa hali tatizo la kuumwa na viungo na pia sikuwa na uwezo wa kusikia katika sikio langu moja.”

Tatizo la kuumwa na viungo lilimfanya ashindwe kunyoosha viungo kulika hali ya kawaida kwani alikabiliwa na hatari ya kuteguka mara kwa mara.

“Hali hiyo ilizidi kuwa mbaya alipokuwa mkubwa… Kila mtu alijua kwamba anakabiliwa na tatizo la kiafya lakini hakuna aliyebaini ni nini hasa.”

Lakini kupitia mitandao ya kijamii Fernanda alifanikiwa kupata ufumbuzi, baada ya kujiunga na kundi Facebook ambalo lilikuwa likijadili ugonjwa wa Ehlers-Danlos.

Fernanda na mama yake katika picha ya kifamilia

Maelezo ya picha,Fernanda Martinez akiwa na mama yake, ambaye anasema aligundua anakabiliwa na tatizo la kiafya tangu alipokua mdogo

“Nilienda kukutana na mtaalamu wa masuala ya jeni. Alinifanyia vipimo vyote na kuthibitisha kuwa nakabiliw na EDS,” alisema msichana huyo aliye na umri wa miaka 22..

Fernanda wakati huo alikuwa na miaka 17 na changamoto zilizotokana na hali hiyo ilikuwa tayari imeathiri vibaya afya yake.

Alikuwa tayari ameathiriwa na hali hiyo, kiasi cha kuwa mfumo wake wa neva ambao unasaidia viungo vingine mwilini kama vile moyo na utumbo ulikuwa umeacha kufanya kazi .

“Nilikuwa nikiharisha, kutapika na kuumwa na tumbo vibaya sana,” anakumbuka.

“Lakini nilikuwa najua jina ya kila kitu kilichokuwa kikinifanyikia. Nilikuwa nikiwaelezea madaktari na watu wengine kile kilichokuwa kikinitatiza.”

Ugonjwa wa Ehlers-Danlos sana sana huathiri uzalishaji wa protini ambao unasaidia kuimarika kwa viongo vya mwili kama vile mifupa, ngozi na misuli inayounganisha viungo vya mwili kama vile mikono na miguu.

“Misuli inayoonganisha viungo hivyo ni hafifu hali ambayo inafanya mishima midogo ya damu kukatika kirahisi,” Fernanda anasema.

Plates with several types of food

Maelezo ya picha,Fernanda swakati mwingine anatamani kula lakini hawezi kufanya hivyo

Je anaweza kula chochote?

“Siwezi kula wala kunywa chochote,” anasema.

“Viungo vyangu vya ndani na misuli imedhoofika kutokana na ugonjwa huu. Mfumo wangu wa neva, ambao unasaidia katika shughuli za usagaji chakula, umuathiriwa.”

“Lakini sijahisi njaa kwa muda mrefu, kwasababu njaa hutegemea na hali katika utumbo na wangu haufanyi kazi tena,

Anasema kuwa wakati mwingine anatamanI kula chakula. Na hilo likitokea, anatafuna chakula na kukitema badala ya kumeza.

“Lakini siku hizi nafanya hivyo kama ada. Kwa mfano, kujumuika na mama yangu wakati wa chakula cha mchana ili asijihisi upweke mezani,” Fernanda anaongeza.

Fernanda alianza kupata changamoto ya kula mwaka 2016 hali ambayo ilimfanya kukubwa na ukosefu mbaya wa lishe bora mwilini

“Nilikuwa nikijaribu kidogo kula lakini hali ilizidi kuwa mbaya.”

Fernanda

Maelezo ya picha,“Lakini sijahisi njaa kwa muda mrefu, kwasababu njaa hutegemea na hali katika utumbo na wangu haufanyi kazi tena”,anasema Fernanda.

Kufikia Mei 2018 alianza kulishwa chakula kupitia mipira iliyokuw aikiingizwa kooni. Ilionekana kuwa suluhisho kwa muda.

“Lakini mwaka mmoja na nusu baadae, mwili wangu ulianza kukataa chochote kinachoingia kupitia mipitra hiyo. Mwili pia uliacha kufunza virutubisho,” Fernanda anakumbuka.

Kufikia mwisho wa mwaka 2019, alilazwa hospitali tena kutokana na ukosefu mbaya wa lishe bora. Madaktari wakavumbua jinsi ya kumsaidia kupata virutubisho hivyo kupitia mfumo wa kusaga chakula na kuingiza mwilini kwake moja kw aamoja kupitia sindano ya kudungwa kwa mshipa.

Je ugonjwa wa Ehlers-Danlos una tiba?

Hakuna tiba ya EDS.

“Tatizo la kuumwa na viungo linaweza kudhibitiwa kwa kukandwa kitaalamu, ili kuzuia madhara zaidi,” anaelezea.

Lakini madaktari wamemwambia Fernanda kuwa tatizo la utumbo wake kushindwa kusaga chakula haitarajiwi kuisha. Hii inamaanisha ataendelea kupata lishe kupitia mishipa maisha yake yote.

Hata hivyo, Fernanda anajaribu kuishi maisha ya kawaida kadiri ya uwezo wake.

“Ninachofanya ili kuishi maisha ya kawaidi ni kucheza michezo ya kielekroniki mitandaoni,” anasema.

“Sijakata tamaa ya maisha kutokana na ugonjwa huu bali nauchukulia kama fursa ya kujifuza kutokana nao.”

Anasema safari yake ya mara kwa mara kumuona ya kutafuta matibabu imemfanya “kupenda” taaluma ya udaktari na amesema hali yake ikiimarika atasomea.

“Hadi wakati huo, naendelea kufanya utafiti kuhusu ugonjwa huuusiokuwa wa kawaida. Ili niweze kuwasaidia wengine wanaokabiliwa nao ili wafahamu ni ugonjwa wa aina gani,” Fernanda anasema.

Chanzo BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents