Fernando Hierro ajiuzuru wadhifa wake kama kocha wa Hispania

Aliyekuwa kocha wa muda wa timu ya taifa ya Hispania, Fernando Hierro amejiuzulu nafasi hiyo baada ya kuongoza taifa hilo kwa muda kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Urusi.

Fernando Hierro arithi mikoba ya Lopetegui kuokoa jahazi la Hispania nchini Urusi

Hierro ambaye ameonekana kama shujaa kwenye taifa la Hispania baada ya kurithi mikoba ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Julen Lopetegui aliyetimuliwa kazi siku moja kabla ya michuano hiyo kuanza kutokana na kutangazwa na kuingia kandarasi na Real Madrid amejiuzuru nafasi yake ya kocha wa muda.

Hispania ambao ni mabingwa wa michuano hiyo mwaka 2010 waliondolewa kwenye mashindano hayo hatua ya 16 bora kupitia mikwaju ya penati dhidi ya wenyeji mwa kombe la dunia Urusi.

Kwa mujibu wa Shirikisho la soka nchini Hispania (RFEF) limesema kuwa Hierro mwenye umri wa miaka 50, ameamua kujiuzuru nafasi yake ba kwenda kutafuta changamoto nyingine nje ya mchezo wa soka.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW