Fichuka waja na mfumo ‘rafiki’ wa kununua movie na nyimbo kwa simu

niki wa pili (533x800)

Hivi karibuni kampuni ya Fichuka ilianzisha huduma mpya na ya kipekee ya kununua kazi za wasanii kwa njia ya simu.
Kwa kuanza kampuni hiyo inauza DVD ya Bum Kubum ya Nikki wa Pili kwa njia ya M-pesa ambapo mnunuzi ataweza kuinunua kwa simu yake na baadaye hutumia code namba atakayoipeleka kwa wakala wa fichuka aliye karibu.

Kwa maana nyingine DVD/CD haiuzwi kwa kupokea pesa mkononi.

Fichuka imesema imeuita mfumo rafiki kwa sababu ni mfumo unaopunguza vichocheo vya wizi wa kazi za wasanii kwa kufanya yafuatayo:

1. Msanii anaunganishwa moja kwa moja na mfumo huu ambapo atakua na akaunti yake ambapo ataweza kuona idadi ya nakala zote alizouza na mahali zilipouzwa.

2. Kwa sababu jamii itafahamu kwamba bidhaa hii haiuzwi kwa kupokea pesa mkononi na anayefanya hivyo ni mwizi, itazuia wauzaji wezi kuuuza bidhaa hii. Muuzaji anatakiwa ahakiki code namba sio kupokea pesa.

3. Bidhaa yeyote inayonunuliwa kupitia mfumo huu ni lazima iwepo kwnye database yetu, kama unayo bidhaa na haipo kwnye database yetu ni dhahiri kwamba umeshiriki katika kumuibia msanii na hatua za kisheria zitachukuliwa,

4. Msanii ana uwezo wa kufahamu kwa majina kila aliyenunua kazi yake na mda alionunua na anaweza pia kuwasiliana na wanunuzi kama atahitaji kufanya hivyo.

5. Kupitia mfumo huu, kazi ya msanii itakua inapatikana kiurahisi kama vocha dukani, kwa hiyo itaongeza uhitaji wa kazi ya msanii na kupunguza mawazo ya kunakili kazi ya msanii.

6. Kwa kuwa wakala hanunui bidhaa, haingii gharama yoyote bali anapata commission itaongeza idadi ya mawakala na kurahisisha upatikanaji.

7. Kwa kuwa pesa anafaidika moja kwa moja na mauzo ya kazi zake, wapenzi wa msanii watapenda kushiriki katika mfumo huu kwa kumsupport msanii na kupata mawasiliano kutoka msanii moja kwa moja.

8. Kwa kuwa itakua inafahamika idadi ya nakala zote zilizouzwa itakua ni rahisi kucontrol soko la mzik na filamu Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents