Burudani

Fid Q aelezea kisa cha Stamina kuachia ‘Wazo la Leo’ badala ya ‘Ushauri Nasaha’

stamina

Leo rapper Stamina aka Kabwela anaachia ngoma yake mpya iitwayo Wazo la Leo aliyomshirikisha Fid Q. Ngoma hiyo imetayarishwa na P-Funk Majani wa Bongo Records.Hata hivyo awali Stamina alikuwa amepanga kuachia ngoma nyingine iitwayo Ushauri Nasaha aliyomshirikisha pia Fareed Kubanda.

Kupitia Twitter, Fid ameelezea kwanini Stamina ameamua kutoa Wazo la Leo badala ya Ushauri Nasaha.Fid ameandika:

WazoLaLeo haikupaswa itoke leo, lakini #STAMINA na timu yake waliamua hivyo baada ya WAKWARE kuilikisha ile #UshauriNasaha mitandaoni.UshauriNasaha ndio iliyopaswa kutoka leo lakin timu ya #STAMINA iliamua kuiweka kando baada ya kukuta wadau wengi wanayo kabla ya muda wake.

Kunasiku #STAMINA alinipigia simu akaniambia ‘Blaza,Hii kitu #UshauriNasaha ni kama Mashahidi wa Yehova tu’ nikamuuliza *unamaanisha nini? STAMINA alisikitishwa sana na kuvuja kwa #UshauriNasaha mitandaoni na hicho kitu kilimstress sana kwasababu aliamini ngoma ishachakachuliwa.

Akaniambia ‘ kwani wewe haujui kama hii ngoma ishasambaa sehemu zote? Kuna watu wengi wanayo na wanatupia mistari ya #UshauriNasaha fesbuk.Nikamuuliza ‘hao watu uliwapa wewe hilo jiwe? Akaniambia ‘ Nope na hapa nilipo nishadata coz sijui wamelitoa wapi, nakutana na bigups tu.

Nikamwambia.. ‘Amshukuru Mungu wake kwa zawadi ya kipaji alichompa’ #STAMINA akaniambia ‘tru story lakini hili suala nimelichukuliaje?Nikamwambia ‘ kuleak kwa #UshauriNasaha ni ishara ya upendo toka kwa mashabiki waliochoshwa na uvumilivu wa ngoma kali toka kwake’

Nikamsisitiza kwa kumwambia ‘ demand ya mziki wake imekua kubwa kupitiliza so ni vyema a-focus zaidi kwenye plan b kwasababu ‘a’ ishadunda.Kisha nikamuuliza ‘ je hauwezi kuandika kali nyingine *kama au *zaidi ya ile?’ Akaniambia ‘hakishindikani kitu’ *nikampa # ya @P_Majani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents